Nafasi Ya Matangazo

January 06, 2024





Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameshiriki Ibada maalum ya kuwakaribisha wanafunzi wa vyuo mbali mbali vya Mkoa wa Dodoma  wa Mwaka wa kwanza na kuukaribisha Mwaka 2024 leo tarehe 06 Januari 2024 katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) usharika wa Kanisa Kuu (CATHEDRAL) uliopo Jijini Dodoma.

Akizungumza na vijana hao Mhe. Senyamule amesema vijana ni kundi la Kimkakati na ukiwa kijana una uwezo wa kufanya kila kitu kwa sababu unakuwa na nguvu ya kufanya kila kitu kwa mda sahihi hivyo kama kijana ni vyema ukazingatia mambo ambayo utanufaika nayo katika ujana wako.

“ Mpo Makao makuu na lengo kuu lililokuleta ni masomo hivyo ni lazima kuzingatia dhumuni na lengo lililokuleta katika Mkoa wa Dodoma na siyo kuingia Katika makundi yasiyofaa.

“Dodoma imeanza mkakati wa kuwa na Ardhi ya Ki mkoa na umekusudiwa mambo makubwa Katika Mkoa na vijana ni tegemeo katika nyanja nyingi ndani ya nchi yetu, inawategemea sana vijana na nguvu kazi ya nchi ni kijana hivyo kama Kijana hakikisha unakua Mtu imara na mwenye hofu ya Mungu” amesema Mhe. Senyamule.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Bw. Elias Kwale, amesema lengo la ibada hiyo ni kuwaandaa Wanafunzi katika kumtegemea Mungu kwenye masomo kipindi wawapo vyuoni na hata baada ya kuingia katika jukumu la kuitumukia Jamii na Serikali, Kuiombea Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kuombea vyuo vikuu nchi nzima, Namna ya kukabiliana na changamoto vyuoni hasa katika ulimwengu huu wa utandawazi kwa kuangalia mazingira tuliyotoka ya kifamilia mahali tunapotaka kwenda pamoja na kusudi la mungu kwenye maisha yetu.

Ibada hiyo iliogozwa na neno kuu lisemalo “BALI NINYI NI MZAO MTEULE, UKUHANI WA KIFALME, TAIFA TAKATIFU,WATU WA MILIKI YA MUNGU” Petro 2:9.
Posted by MROKI On Saturday, January 06, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo