Na Raymond
Mtani BMH.
Imeelezwa kuwa Pombe na Sigara vyaweza kuwa miongoni mwa vyanzo vya Watoto kuzawaliwa na magonjwa yakiwemo magonjwa ya Moyo.
Hayo
yamesemwa na Dkt. Victor Urio, Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto katika
Hospitali ya Benjamin Mkapa, kwamba tafiti nyingi zinaonesha kati ya Watoto
1000 wanaozaliwa hai kote duniani 8 huwa na hitilafu mbalimbali za Moyo.
Shirika la
Afya Duniani (WHO) linakadilia kuwa zaidi ya Watoto 240,000 hufariki kwa
magonjwa ya kuzaliwa nayo yakiwemo ya Moyo kila mwaka kabla ya kufikisha siku 28,
huku zaidi ya 170,000 wakifariki kati ya umri wa mwezi 1 na miaka 5 kwa
magonjwa hayo.
Kama hiyo
haitoshi, WHO inatanabaisha Watoto 9 kati ya 10 wenye magonjwa ya kuzaliwa nayo
wanatoka nchi za zenye Uchumi wa chini na wa kati, nchi za jumhiya ya Afrika
Mashariki zikiwa miongoni mwa nchi hizo.
Dkt. Victor
Urio, anasema takwimu hizo hazipingani na zinazoonekana katika kliniki ya
Watoto ya Hospitali ya Benjamin Mkapa.
“Kwenye kila
mwezi tunaona Watoto kati ya 10 hadi 20 wakiwa na magonjwa ya Moyo ya kuzaliwa
nayo” Alisema Dkt. Urio.
Akiongeza
kuwa kama ilivyo duniani kote Matundu na Mishipa ambayo haijafunga kwenye Moyo ni
miongoni mwa hitilafu zinazowakabili Watoto wengi wanaobainika kuwa na Magonjwa
ya Moyo ya kuzaliwa nayo Hospitalini
hapo.
Ingawa,
wataalamu hawajeweza kubaini sababu halisi za Watoto kuzaliwa wakiwa na hitilafu
kwenye Moyo, yako mazingira yanayoongeza uwezekano wa mama kujifungua mtoto
mwenye hitilafu za Moyo.
“Kutumia pombe na Kuvuta Sigara wakati wa Ujauzito, ni tabia zinaongeza uwezekano wa mama kujifungua mtoto mwenye hitilafu katika Moyo” Alisema Dkt. Urio.
Mbali na
tabia hizo, kuchelewa kuanza Kliniki kwa mama mjamzito kunakomchelewesha kuanza
matumizi ya vidonge vyenye madini ya Foliki humuweka mjamzito katika hatari ya
kujifungua mtoto mwenye hitilafu ya Moyo.
“Vile vidonge
vya Foliki vinahusika katika kujenga maumbile ya mtoto” alisema Dkt. Urio na kuongeza
kuwa, ziko sababu za kurithi na za kimaumbile, na wakati mwingine maambukizi anayoyapata
mama wakati wa ujauzito kama vile virusi vya Rubella yaweza kuwamweka katika
hatari ya kujifungua mtoto mwenye hitlafu kwenye Moyo” Amesema Dkt. Urio
Tanzania ni
miongoni mwa nchi zinazopambana kuimarisha sekta ya Afya kwa kasi kubwa kwa
kuhakikisha huduma za Afya zinapatikana jirani na mazingira wanayoishi wananchi
wake, lakini vilevile kuboresha utoaji wa huduma kwa kupeleka wataalamu na
vifaa tiba.
Kama haitoshi,
serikali imeleta mfumo wa Bima ya Afya kwa wote, jambo litakaloleta unafuu wa
gharama za matibabu.
Imeelezwa kuwa Pombe na Sigara vyaweza kuwa miongoni mwa vyanzo vya Watoto kuzawaliwa na magonjwa yakiwemo magonjwa ya Moyo.
“Kutumia pombe na Kuvuta Sigara wakati wa Ujauzito, ni tabia zinaongeza uwezekano wa mama kujifungua mtoto mwenye hitilafu katika Moyo” Alisema Dkt. Urio.
0 comments:
Post a Comment