Na Issa Mwadangala
Jamii imeaswa kuendelea kujenga na kuimarisha misingi imara ya malezi na makuzi ya watoto ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya Ushoga, Usagaji, uhalifu pamoja na vitendo vingine vilivyo kinyume na mila na tamaduni za Kiafrika.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya, Novemba 27, 2023 wakati wa mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari ya Bweni iitwayo God’s Bridge iliyopo mkoani Songwe.
Alisema ''inashangaza kuona mtoto akirudi nyumbani usiku wa manane na mzazi au mlezi akimfungulia mlango na bila kuhoji anakotoka jambo ambalo si la kawaida na ni dalili ya mzazi au mlezi kupoteza uelekeo hasa kwenye suala la malezi'' pia alisisitiza wazazi kusimama imara kuhakikisha mtoto anatimiza wajibu wake na kuelekezwa hatari zinazoweza kujitokeza na kuharibu maisha yake ya baadae.
Akiwa mgeni rasmi katika mahafali hayo pia Kamanda Mallya, aliweza kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya kununua Televisheni, itakayotumika shuleni hapo kama sehemu ya kujifunzia ambapo pia alikabidhi vitabu mbalimbali vya sheria kama Sheria ya Mtoto inayohusu Kanuni na Usalama wa Mtoto amekabidhiwa sheria hiyo ili kuhakikisha zinasimamiwa ikiwa ni pamoja na watoto kutendewa haki.
No comments:
Post a Comment