Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Bi Susan Liautaud (mwenye barakoa) wakiwa na mototo wa mmoja wa wazazi wa watoto wanaosoma skuli ya Maandalizi ya Awali ya Kikaangoni Wilaya ya Maagharibi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakifurahia mchoro wa mwanafunzi katika skuli ya Maandalizi ya Awali ya Kikaangoni Wilaya ya Maagharibi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Bi Susan Liautaud (mwenye barakoa) na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe Lela Mohamed Mussa (kushoto kwa Dkt Kikwete) wakiangalia wanafunzi katika darasa la skuli ya Maandalizi ya Awali ya Kikaangoni Wilaya ya Magharibi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakilakiwa kwa burudani waliopowasili skuli ya Maandalizi ya Awali ya Kikaangoni Wilaya ya Magharibi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ujumbe wake wakiondoka Skuli y Msingi ya Kisiwandui.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, na ujumbe wao wakiwa Skuli ya msingi ya Kisiwandui mjini Magharibi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Bi Susan Liautaud wakiwa na Walimu wa Skuli ya Msingi ya Kisiwandui.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe Lela Mohamed Mussa akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, na ujumbe wao baada ya ziara ya kutembelea Skuli za Visiwani leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti na wajumbe wa bodi katika picha ya Pamoja baada ya kukagua Skuli ya Msingi ya Kisiwandui.
*************
Na Mwandishi Maalumu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu
Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na
Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, leo wametembelea na kukagua
skuli zinazopata ufadhili na shirika hilo.
Katika ziara ya leo ujumbe huo mzito wa GPE ulitembelea na kukagua skuli
ya Maandalizi ya ya Kikaangoni pamoja na
Skuli ya msingi ya Kisiwandui, ukiwa umeongozana na wenyeji wao Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe Lela Mohamed Mussa, na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi, Mhe Suzan Peter Kunambi.
Huo ni mwendelezo wa ziara ya viongozi na wajumbe wa bodi ya GPE
kutembelea miradi mbalimbali yya bara na visiwani kabla Dkt. Kikwete, akiwa
mwenyekiti wa Bodi hio ataongoza vikao vya Shirika hilo hapa Zanzibar kuanzia
leo 4 hadi 6 Disemba, hiyo ikiwa ni mara
ya kwanza kwa Shirika hilo la kimataifa kufanya vikao vyake vya bodi barani
Afrika na nje ya Marekani na Ulaya.
GPE iliyoanzishwa mwaka wa 2002, ni Shirika lililoundwa na mataifa
Tajiri duniani ya G& na linasimamiwa na Benki ya Dunia, kufadhili maendeleo
ya elimu katika nchi zinazoendelea.
Majukumu ya GPE ni pamoja na kusaidia serikali za nchi
zinazoendelea kufanya mabadiliko ya kimfumo na kuoanisha rasilimali na ufadhili
ili kutoa elimu bora kwa watoto Wote, kuinua viwango vya kujifunza na
kukabiliana na changamoto mpya nchini.
Kwa mujibu wa Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza
GPE, shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya Dola za
Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia
sekta ya elimu bara na visiwani.
Majuzi GPE imetiliana saini na Serikali ya makubaliano ya kutoa dola za
Kimarekani milioni 85 (takriban shilingi 213, 775, 085,
000.0) kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya walimu nchini.
No comments:
Post a Comment