Katika kuadhimisha Siku ya Wanaume Duniani, Benki ya CRDB imefanya semina ya siku moja kwa wafanyakazi wake wanaume ili kuwajengea uwezo katika masuala ya kisaikolojia, kimwili na kijami.
Semina hiyo iliendeshwa na madaktari pamoja na wanasaikolojia, na kufanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam.
Licha ya kuwajengea wafanyakazi uwezo wa kusimamia mambo yao binafsi, pia imelenga kuongeza morali na kuwatia moyo wa kujituma zaidi kila wanapowahudumia wateja ili kukidhi mahitaji na matarajio yao ya kifedha.
Siku ya Wanaume Duniani huadhimishwa kila ifikapo Novemba 19 ya kila mwaka ili kutoa nafasi kwa wanaume kujadili maendeleo yao binafsi pamoja na ya familia zao na kutafuta suluhu ya changamoto wanazokabiliana nazo.
Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, wafanyakazi wa Benki ya CRDB wamepitishwa kwenye mada kadhaa ikiwamo afya ya akili, afya ya uzazi, familia na malezi pamoja na saikolojia ya jamii.
Mjadala huo umelenga kuwajengea uwezo wa kurahisisha maisha yao ndani ya ndoa, maisha binafsi pamoja na jinsi wanavyochangamana na jamii bila kusahau maisha yao wakiwa kazini.
Mtaalamu wa Masuala ya Saikolojia nchini, Dkt. Ellie Waminian akizungumza katika semina ya siku moja kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB wanaume ili kuwajengea uwezo katika masuala ya kisaikolojia, kimwili na kijami, iliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ambaye ni Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo akizungumza katika semina ya siku moja kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB wanaume ili kuwajengea uwezo katika masuala ya kisaikolojia, kimwili na kijami, ikiwa ni sehemu kuadhimisha Siku ya Wanaume Duniani, iliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam.
Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile akizungumza katika semina ya siku moja kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB wanaume ili kuwajengea uwezo katika masuala ya kisaikolojia, kimwili na kijami, ikiwa ni sehemu kuadhimisha Siku ya Wanaume Duniani, iliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Timothy Fasha akizungumza katika semina ya siku moja kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB wanaume ili kuwajengea uwezo katika masuala ya kisaikolojia, kimwili na kijami, ikiwa ni sehemu kuadhimisha Siku ya Wanaume Duniani, iliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi Benki ya CRDB waadhimisha Siku ya Wanaume Duniani
0 comments:
Post a Comment