November 27, 2023

TULINDE VYANZO VYA MAJI KWA WIVU MKUBWA

Dkt. Biteko awavaa waharibifu wa Mazingira, akemea ukataji miti hovyo

Na. Mwandishi Maalum, Arusha

Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati nchini Dkt. Dotto Mashaka Biteko, amewataka watanzania kuwa walinzi wa dhidi ya uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji na kukemea vitendo vya ukataji hovyo wa miti na aina zote za uharibifu wa mazingira huku akiwaagiza TANESCO kuwa mstari wa mbele katika mapambano ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji kwa kuzingatia ukweli kuwa maji ni moja ya chanzo kikuu cha kuzalisha umeme nchini na mapema mwakani mara tu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bwawa wa Nyerere litakalozalisha Megawatt 2115 maji yatakuwa rasilimali namba moja ya uzalishaji umeme nchini

‘’Watanzania miundombinu hii tunayopewa na serikali yetu, moja tuna wajibu wa kuilinda, vyanzo vyetu vya umeme pamoja na gesi tuna chanzo kikubwa kitakachozidi gesi baada ya muda si mrefu, chanzo cha maji nah ii ni kutokana na uwepo wa bwawa la mwalimu Nyerere vyanzo vya maji visipolindwa na kwa mfumo wa Maisha tunaoishi hii miradi yote itakuwa kila kiangazi tunakuja kupeana Habari za mgao wa umeme na lawama zote zitahama kutoka kwa wanaoharibu mazingira zitakwenda kwa TANESCO na watu hawatamuona aliyekata mti, na watu hawatamuona aliyeharibu chanzo cha maji, watamuona TANESCO ambaye amegawa umeme’’, 

‘’lakini kuna wenzetu wanakata miti, wanaharibu mazingira, maji yakikosekana, leo tunazungumza umeme miaka ijayo tutakuwa na stress ya maji, maji kwa huduma mbalimbali, ya kunywa, ya kilimo nakadharika ni lazima tulinde vyanzo vya maji,tukishakuvulinda hivyo vyanzo vya maji sisi tunabadilisha kuwa umeme, leo kule Tanga hale ambako na kwenyewe tunazalisha umeme kwa sababu ya uwepo wa maji mengi kule kumeimarika , upungufu uliokuweko hale umepungua kwa sababu ya uwepo wa maji’’

‘’Leo tunavyozungumzayako maeneo ambayo ni vyanzo kabisa vya maji lakini kuna wenzetu wanakata miti, wanaharibu mazingira’’

‘’TANESCO, kwenye habari ya kulinda mazingira, kwenye habari ya kulinda miundombinu yenu msibaki kwenye siti ya kusubiri, ninyi nuwe mbele, shirikianeni na wizara ya mazingira, shirikianeni na NEMC wote kwa pamoja tusimamie mazingira ya nchi hii tusimamie miundombinu’’.

‘’nitoe wito kwetu wote watanzania tuvilinde vyanzo vya maji kwa wivu mkubwa,wazee wetu ambao walikuwepo kabla yetu walivilinda vyanzo hivyo kwa wivu mkubwa ndio maana leo tunaviona, tunavitumia’’.

‘’hivi sisi hatuoni deni la kuacha vyanzo hivi vya maji kwa ajili ya wajukuu wetu na wao wakute mahali pazuri kama ambavyo tumekuta sisi kwa wazee wetu walituachia, kwanini haituumi?, kwanini haitushughulishi?, anakata mtu mti anapita mtu anasikia shoka na wala haimsumbui kwamba kwanini mti ule unakatwa huku akijua mti ule kukatwa utasababisha mti wa pili kukatwa, watatu kukatwa na baadae kuwa na jangwa na baadae kuwa na ukame’’.

‘’Tulinde vyanzo vyetu, tuvisimamie, akitokea mtu anataka kuturudisha nyuma isiwe kazi ya serikali, na serikali itakapotokea inawashughulikia wanao haribu mazingira tusitokee tena huku wengine tukaanza kuwapigia debe wale ambao wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria sisemi watu waonewe kwa sababu kuna watu wabaya wanaweza kutumia fursa hiyo lakini wale wanaoharibu mazingira washughulikiwe kwa maslahi ya kuyalinda mazingira yetu’’.

Amesema Dkt. Dotto Biteko, Novemba 26, 2023 wakati alipokagua kituo cha umeme cha Lemuguru mkoani ambacho ujenzi wake ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa njia kuu ya umeme ya msongo wa kV 400 kutoka Singida mpaka Namanga kuelekea Kenya ( Kenya- Tanzania Power Interconnection Project (KTPIP). ‘.

No comments:

Post a Comment