Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule akipokea ngao maalum kutoka kwa Bw.Ekuzi Elias (Mzalendo Halisi) ikiwa na ujumbe maalum wa pongezi kwa Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson kufuatia ushindi wake wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa wabunge Duniani (IPU).
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule Novemba 17,2023 kwaniaba ya spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson amepokea pongezi za kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa wabunge Duniani (IPU) kutoka kwa Bw.Ekuzi Elias (Mzalendo Halisi).
Bw.Ekuzi amefikisha pongezi zake kwa kutembea kwa miguu kwa takribani siku tano kutoka Mkoa wa Morogoro hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma huku akiwa na bango lililoandikwa ujumbe wa kutoa pongezi kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson.
Dkt.Tulia Ackson alichaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Oktoba 27,2023 huku akiwa ni Rais wa 31 na ni mwanamke pekee kuchaguliwa Barani Afrika.
No comments:
Post a Comment