Nafasi Ya Matangazo

October 26, 2023

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri Mpwapwa yenye Lengo la kutathmini utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 




Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma, wameaswa  kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kuwezesha miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo kuwa na tija na ufanisi mkubwa.

Rai  hiyo imetolewa  tarehe 25 Oktoba, 2023 na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Ally Gugu wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri hiyo yenye Lengo la kutathmini utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

"Mfanye kazi kama timu moja kwa kushirikianisha mambo na muwe na  muunganiko na huo ndio upendo , taarifa za miradi zinapo Kuja mshirikishane isiwe ya mtu mmoja " ameeleza Gugu.

Aidha, Amesisitiza suala la usimamizi wa mapato ya Halmashauri na kusema ni lazima kusimamia kwa uaminifu fedha zikusanywe na kupelekwa sehemu husika pamoja na kutafuta mbinu  nyingine za vyanzo vya mapato na zaidi ya yote ni kusimamia kwa  uaminifu  matumizi ya fedha za Serikali.

"Lazima muwe na mkakati madhubuti ya kusimamia mapato yaliyopo lakini kuzalisha vyanzo vipya vya mapato na kuvisimamia ,fedha zikusanywe na zipelekwe kwa wakati sehemu husika kwa kuzingatia sheria na taratibu za matumizi husika " Ameongeza'

Katibu Tawala Mkoa pia amegusia suala la afya na kuwataka watumishi kuchukua tahadhari kwenye afua za maradhi ili kujiepusha na yale yanayo epukika pamoja na kuzingatia Lishe bora.

Kwa upande wake, Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpwapwa, Bi.Mwanahamisi Ally  amemuahidi Katibu Tawala Mkoa kutekeleza maelekezo yote aliyotoa na kumuhakikishia  kutoa taarifa kwa wakati.

Awali Bw. Gugu alianza na  kikao cha pamoja  cha tathmini ya miradi na vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri na Wakuu wa Idara kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na baada ya hapo  alifika katika Shule  mpya ya Sekondari ya Kimagai, Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa na Shule ya Sekondari ya Mazae kwa ajili ya ukaguzi na utekelezaji wa maendeleo ya miradi.

Pia, miradi hiyo mitatu kwa maana ya  ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kimagai, ujenzi wa Jengo la Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya, vyumba 9 vya madarasa, mabweni 4 na matundu kumi na manne ya vyoo unaogharimu zaidi ya shilingi Billioni moja.
Posted by MROKI On Thursday, October 26, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo