Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka akisisitiza jambo kwa wadau wa kilimo katika mikoa ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania pamoja na mambo mengine amewahimiza kuwa karibu sana na Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) ili mikakati ya kuzalisha mazao ya kilimo na biashara itekelezwe kwa ufanisi na ndoto ya Rais Samia Hassan ya Tanzania kulilisha Bara la Afrika
Na Mwandishi Wetu, Njombe
Wadau wa kilimo katika mikoa ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania wamehimizwa kuwa karibu sana na Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) ili mikakati ya kuzalisha mazao ya kilimo na biashara itekelezwe kwa ufanisi na ndoto ya Rais Samia Hassan ya Tanzania kulilisha Bara la Afrika itimie.
SAGCOT ndiyo
taasisi inayotambua wadau wa kilimo
katika ushoroba wa kusini mwa Tanzania na kuratibu ushirikiano baina yao ili
uzalishaji wa mazao ya kilimo na
biashara uwe wenye tija na kuboresha maisha ya wakulima wadogo kwa kutumia
sayansi na teknolojia katika kulima mazao.
Akiongea katika
mkutano wa siku mbili wa wadau wa kilimo kutoka taasisi za sekta binafsi na
umma zilizomo katika Kongani ya Ihemi,
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amewataka wadau hao kushirikiana na
SAGCOT katika kuhamasisha wakulima kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula na
biashara ili ziada ya mazao ya chakula iwe
kubwa na ilishe Bara la Afrika ifikiapo 2030. Aidha ameishauri SAGCOT ielewe ndoto ya Rais
Samia kwani ina uzoefu mkubwa katika kuwaingiza Watanzania katika kilimo.
Mtaka
alisema kuzalisha ziada kubwa ya chakula
kwa kutumia mikakati iliyo, ikiwemo utoaji wa mbolea ya ruzuku, ni dhamira ya serikali ya kulisha Afrika
ifikapo 2030. “Kulisha Afrika ni ndoto ya Rais Samia na ni dhamira ya serikali
anayoiongoiza,” alisema, na kuongeza kuwa dhamira ya serikali inaonekana kwa
kuwawezesha wakulima kwa kutumia mikakati mbalimbali ikiwemo utoaji wa mbolea
za ruzuku.
‘’Political will
(dhamira ya kisiasa) sasa hivi ya kukuza kilimo ni ya rais mwenyewe na ni kubwa
mno. Mnaona ameishasema visima eflu 68 vichimbwe kwabajili ya umwagiliaji
lakini pia mabwawa yachimbwe; na pesa zimeisha tolewa kwa ajili kuanza
uchimbaji. Haya ni matamanio makubwa ya
kiongozi wa nchi na sisi SAGCOT ni lazima tumulewe vizuri Rais, tusaidie
matamanio haya kufikiwa,’’alieleza Mtaka.
Alisema SAGCOT
wamesaidia watu wengi kuingia katika shughuli za kilimo na kwamba kuongezeka
kwa uzalishaji wa maparachichi na viazi mviringo ni ushahidi wa kuongezeka kwa
uzalishaji tangu SAGCOT walipoanza
kuwahudumia wakulima mwaka 2015.
Mkuu huyo wa
Mkoa aliwataka wadau hao kutafuta
majawabu ya changamoto zilizopo kwenye sekta za kilimo na ufugaji na
kusema dhamira ya kukuza kilimo
inajitokeza katika kuwawezeha wakulima kuhusu mbolea, uchimbaji wa
visima na utengenezaji wa mabwawa ya kumwagilia mazao na mradi wa Jenga Kesho
iliyo Bora (BBT). BBT inawalenga vijana
wengi ili wazalishe kisasa na kupunguza
changamoto ya ajira kwa vijana.
Aidha amewataka
viongozi kuunganisha taasisi binafsi nawakulima na viongozi wa serikali kuhamasisha shughuli za kilimo.
‘’Zamani
wakilima walikua wanapata gunia 40 za viazi mbatata. Lakini sasa watu wanavuna mpaka gunia 200.
Hii ni kazi nzuri inayofanywa na ninyi
wenzetu Sagcot. Hii ni tija kubwa na hongereni, ’’alisema Mtaka
Awali Mkuu wa
Maendeleo ya Kongani na Ubia wa SAGCOT, Bi Maria Ijumba akiwasilisha taarifa ya
makubaliano yaliyofanyIka mwaka 2022 alisema kuwa ndani ya mwaka mmoja
limekuweko ongezeko kubwa katika nyanja za ajira, uzalishaji na uwekezaji, na
kuwa sekta ya kilimo imesaidia kundi kubwa la Watanzania wameshinda umasikini baada ya kuingia kwenye kilimo na
ufugaji.
Amesema
tathimini ya mwaka 2022 inaonyesha kuwa wakulima wadogo wa mazao ya biashara
wameongezeka mara 8 kutoka laki moja mpaka kufikia 847,385.
Na Mwandishi Wetu, Njombe
Wadau wa kilimo katika mikoa ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania wamehimizwa kuwa karibu sana na Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) ili mikakati ya kuzalisha mazao ya kilimo na biashara itekelezwe kwa ufanisi na ndoto ya Rais Samia Hassan ya Tanzania kulilisha Bara la Afrika itimie.
No comments:
Post a Comment