Nafasi Ya Matangazo

October 22, 2023

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia Tanzania Dkt. Beatrice Lyimo Akizungumza leo Oktoba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Vituo vya Ubunifu na Utafiti vilivyowezeshwa na COSTECH.

Patrick Kitosi Mkurugenzi wa Kampuni ya Utafiti na ubunifu ya Sensor Tanzania Limited ya jijini Dar es Salaam akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari wakati walipotembelea katika ofisi zake kuona namna wanavyoweza kuvuna sumu ya nyuki kwa teknolojia waliyoibuni wenyewe.

Patrick Kitosi Mkurugenzi wa Kampuni ya Utafiti na ubunifu ya Sensor Tanzania Limited ya jijini Dar es Salaam akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari  jinsi kifaa maalum cha kuvuna sumu ya Nyuki kinavyofanya kazi wakati walipotembelea katika ofisi zake kuona namna wanavyobuni vifaa hivyo.

..............................

NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM

Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejipanga kutoa fedha kwa wakimama kwa ajili ya kufanya utafiti wa kisayansi katika upande wa usalama wa chakula.

Akizungumza leo Oktoba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Vituo vya Ubunifu na Utafiti vilivyowezeshwa na COSTECH, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia Tanzania Dkt. Beatrice Lyimo, amesema kuwa kwa mwaka huu wa fedha wanatarajia kutoa fedha kwa wakimama ili waweze kufanya utafiti.

Dkt. Lyimo amesema kuwa lengo ni kuendelea kutoa fedha kwa ajili wabunifu pamoja na watafiti ili kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa.

"Wanaume wengi wanapata fursa ya kukopa fedha na kufanya utafiti tofauti na wakimama" amesema Dkt. Lyimo.

Amebainisha kuwa asilimia 70 wanaume wamekuwa wakipata fursa ya kupata mkopo na kufanya utafiti.

Dkt.Dkt. Lyimo ameeleza kuwa bado hawajaaza kutoa fedha, huku akieleza kuwa watatumia njia mbalimbali ikiwemo mashindano ya kibunifu ili kuwapata wakinamama wabunifu.

Bw. Geofrey Rwechungura MKurugenzi wa Kampuni ya Agro Company Limited akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari wakati wa ziara na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Vituo vya Ubunifu na Utafiti vilivyowezeshwa na COSTECH.

Bw. Geofrey Rwechungura Mkurugenzi wa Kampuni ya Agro Company Limited akiwaonesha wahariri wa vyombo vya habari namna mashine ya kutengeneza chakula cha Samaki inavyofanya kazi wakati wa ziara na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Vituo vya Ubunifu na Utafiti vilivyowezeshwa na COSTECH.

Baadhi ya wafanyakazi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  Tanzania COSTECH wakiwa ni miongoni mwa ujumbe uliofanya ziara pamoja na Wahariri wa vyombo vya habari kujionea vituo vya ubunifu na utafiti vinavyofanya kazi.

Meneja wa Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) Dkt. Charles Mayemba akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari wakati wa ziara na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Vituo vya Ubunifu na Utafiti vilivyowezeshwa na COSTECH mjini Kibaha.

Meneja wa Meneja wa Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) Dkt. Charles Mayemba akiongozana na wahariri wa vyombo vya habari wakati wa ziara na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Vituo vya Ubunifu na Utafiti vilivyowezeshwa na COSTECH mjini Kibaha.

Dkt Richard Mwakapuja Mtafiti na Mchambuzi mwandamizi wa Maabara Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) Kibaha akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari wakati wa ziara na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Vituo vya Ubunifu na Utafiti vilivyowezeshwa na COSTECH mjini Kibaha.

Dkt Richard Mwakapuja Mtafiti na Mchambuzi mwandamizi wa Maabara Meneja wa Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) Kibaha akionesha baadhi ya mashine za kufanyia uchunguzi wa kimaabara  kwa wahariri wa vyombo vya habari wakati wa ziara na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Vituo vya Ubunifu na Utafiti vilivyowezeshwa na COSTECH mjini Kibaha.

Picha ya pamoja.

Posted by MROKI On Sunday, October 22, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo