Aliyekuwa Kamishna wa Polisi Jamii , Kamishna wa Polisi Dkt. Mussa Ali Mussa ambaye ameteuliwa kuwa RAS mkoa wa Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Makatibu
Tawala wa Mikoa wapya 07 na kuwahamisha vituo vya kazi Makatibu Tawala wa Mikoa
10 na wengine 09 kubakia kwenye vituo vyao kama ifuatavyo:-
A) MAKATIBU TAWALA WA MIKOA WAPYA
Kamishna
Dkt. Mussa Ali Mussa - Ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.
Prof.
Godius Walter Kahyarara – Ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Alikuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
Mhandisi
Leonard Robert Masanja – Ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa. Alikuwa
Mkufunzi wa Chuo cha TANESCO Mkoani Dar es Salaam.
Toba
Alnason Nguvila – Ameteuliwa kuwa Katibu
Tawala Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa
Wilaya ya Muleba, Mkoani Kagera.
Elikana
Mayuganya Balandya – Ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na
Mipango.
Prof.
Siza Donald Tumbo – Ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga. Alikuwa
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo.
Dkt.
John Rogath Mboya – Ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora. Alikuwa
Kamishna wa Idara ya Bajeti katika Wizara ya Fedha na Mipango.
B) WALIOHAMISHWA VITUO VYA KAZI:
Missaile Albano Musa – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha.
Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.
Rehema Seif Madenge – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es
Salaam. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi.
Hassan Abbas Rugwa – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi.
Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam.
Ngusa Dismas Samike – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi.
Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza.
Msalika Robert Makungu – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mara.
Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora.
Msovera Albert Gabriel – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma.
Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mara.
Rodrick Lazaro Mpogolo – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya.
Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi.
Zuwena Omari Jiri – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Pwani.
Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.
Happiness William Seneda – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa
Songwe. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa.
Rashid Kassim Mchata – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa.
Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma.
C) AMBAO WANAENDELEA NA VITUO VYA KAZI:
Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa
Dodoma
Karolina Albert Mthapula – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa
Manyara.
Abdallah Mohamed Malela – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.
Judica Haikale Omary – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe.
Willy Lugahyulula Machumu – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa
Kilimanjaro.
Steven Mashauri Ndaki - Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma.
Dorothy Aidan Mwaluko - Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida.
Prisca Joseph Kayombo - Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu.
Pili Hassan Mnyema - Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga.
Uapisho utafanyika Ikulu
Chamwino, Dodoma tarehe 1, Agosti, 2022.
No comments:
Post a Comment