Jeshi la polisi mkoani Tabora linamshikilia Mbalu Mwagembe kwa tuhuma ya kumlisha dawa ya kienyeji mume wake aliyopewa na mganaga kwa lengo la mumewe kuacha ulevi uliopitiliza lakini dawa hiyo inaiwadawa ilikuwani sumu iliyopoteza maisha ya mwanaume huyo.
Akitoa taarifa kwavyombovya habari jana Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Tabora ACP. Safia Jongo (pichani) alimtaja mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Talibona Nyerere ( 47 ) alilishwa dawa hiyo na mke wake mdogo.
Alisema kwamba tukio hilo lilitokea septemba 3 mwaka huu katika Kitongoji Cha Mtakuja Kijiji Cha Mwanzwilo kata ya Igusule Tarafa ya Mwakalunde Wilayani Nzega mkoani Tabora .
Alisema kwamba mwamke huyo Mbalu Magembe baada ya kurejea nyumbani akiwa amelewa mume wake Kama ambavyo imekuwa kawaida yake kumpa dawa hiyo ili aweze kuacha ulevi wa pombe.
Alisema kwamba ilikuwa ni maelekezo ya mganga wa kienyeji kwamba itasaidia mwanaume huyo kupunguza pengine kuacha kabisa ulevi .
Acp Safia alisema kwa baadaya kufanya mahojiano na mtuhumiwa huyo alimtaja wa mtaja mganga jina lihifadhiwa na na anashikiliwa na jeshi hilo.
Hata hivyokamanda huyo wa polisi halitoa tadhari kwa wananchi kuwa makini na waganga hao jadi ambao wamepelekea kusababaisha kifo mtu huyo.

No comments:
Post a Comment