August 02, 2021

WANAHABARI TANZANIA WAPATA VHANJO YA UVIKO 19

 

Mpigapicha Felix Fidelix akichomwa Chanjo ya UVIKO 19.
Khalfan Said wa K-Vis Blog akichomwa Chanjo.
Mbaraka Islam akichomwa Chanjo 
Sehemu ya wahariri na Waandishi waliojiyokeza kuchomwa Chanjo ya UVIKO 19
WAHARIRI na waandishi wa habari wamepatiwa chanjo ya kujikinga dhidi ya maradhi ya UVIKO 19 katika zoezi lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Agosti 2, 2021.

Zoezi hilo lililoratibiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile lilikuwa la hiari na idadi kubwa ya wahariri na waandishi walijitokeza kupokea chanjo hiyo ya Johnson and Jonson iliyowasili nchini Julai 24, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua zoezi lachanjo ya hiari kitaifa Julai 28, Ikulu jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wananchi kuwa chanjo hiyo ni salama.
Shehena ya chanjo hiyo dozi Milioni moja na ushee imetolewa na serikali ya Marekani kama msaada chini ya Mpango wa COVAX, ambapo Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima alisema, katika awamu ya kwanza chanjo hiyo itayahusu makundi maalum yaliyo mstari wa mbele, ambayo ni pamoja na watoa huduma za afya, vikosi vya ulinzi na usalama lakini pia makundi ambayo yako kwenye hatari ya maambukizi ya Covid 19 kama vile watu wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea na wenye maradhi ya muda mrefu.
Balile aliishukuru Wizara ya Afya kwa kutoa kipaumbele kwa waandishi wa habari kwani nao ni watu walio katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo kutokana na mazingira ya kazi wanazozifanya ambazo ni pamoja na kukutana na wagonjwa, na watu mbalimbali katika maeneo mbalimbali.
“Tungeomba zoezi hili pia lifanyike kwa waandishi wa habari walio mikoani kwani nao wanakabiliwa na hatari kama ya walio chanjwa leo.” Alisisitiza Balile. 
SOURCE: K-VIS BLOG

No comments:

Post a Comment