Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua pamba ambayo imechambuliwa na kufungwa tayari kwa kuuzwa wakati alipozindua kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS Investment Company Limited kilichopo ifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi Agosti 26, 2021. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Emmanuel Njalu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS Investment Company Limited kilichopo ifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi, Emmanuel Njalu (kulia) wakati alipozindua kiwanda hicho, Agosti 26, 2021. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mwananvua Mrindoko.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uchambuaji wa pamba kutoka kwa Emmanuel Njalu (wa pili kushoto) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS Investment Company Limited kilichopo Ifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi baada ya kuzindua kiwanda hicho, Agosti 26, 2021.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua kiwanda cha kuchambua pamba cha NGSInvestment Company Limited kilichopo Kifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi, Agosti 26, 2021. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda, Emmanuel Njalu, wa tatu kulia ni Mbunge wa Mpanda V ijijini, Suleiman Kakoso na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Katavu, Beda Katani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS Investment Company Limited kilichopo Kifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi wakati alipowasili kiwandani hapo kuzindua hiwanda hicho, Agosti 26, 2021. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda, Emmanuel Njalu na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua, Mrindoko.
*********
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua kiwanda cha kuchambua pamba cha Kampuni ya NGS Investment Ltd na kuwataka wakulima watumie fursa ya uwepo wa kiwanda hicho kwa kuongeza mashamba kwa sababu kinawapa uhakika wa soko la zao hilo.
Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuajiri watumishi katika sekta ya kilimo na kuwasambaza kwenye maeneo mbalimbali nchini hususan ya vijijini kwa ajili ya kuwasaidia wakulima kuweza kulima mazao yao kwa kufuata mbinu bora za kilimo na kuongeza tija.
Waziri Mkuu amezindua kiwanda hicho leo (Alhamisi, Agosti 26, 2021) kilichopo katika kijiji cha Ifukutwa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi. Amesema zao la pamba ni miongoni mwa mazao ya kimkakati, hivyo Serikali itaendelea kulisimamia katika hatua zote.
Amesema mbali na kiwanda hicho kutoa soko la uhakika kwa wakulima wa pamba pia manufaa mengine ni kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka kiwanda kupata ajira za moja kwa moja na za muda, hivyo kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira.
Mheshimiwa Majaliwa amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuinua uchumi wa nchi kwa kuendeleza ujenzi wa miundombinu ili itumike na wananchi kusafirisha mazao na kusambaza bidhaa mbalimbali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya NGS, Njalu Silanga amesema ujenzi wa mradi wa kiwanda hicho ulianza Januari 2020 na unatarajiwa kugharini Dola za Marekani milioni mbili sawa na shilingi bilioni 4.5.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa kiwanda hicho kinauwezo wa kuchakata tani 50,000 za pamba kwa msimu mmoja ila uzalishaji wa pamba katika mkoa wa Katavi bado uko chini ikilinganishwa na uwezo wa kiwanda kutokana na upatikanaji wa pamba ghafi.

No comments:
Post a Comment