Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la korosho la Bw. Jumanne Kilegele lililopo Kagungu wilayani Tanganyika, Agosti 26, 2021. Yupokatika ziara ya kikazi mkoani Katavi.
Wakati akitembelea Shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 40 na mikorosho 1,080, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika ukutane na mkulima huyo kwa ajili ya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa zao hilo.
Alisema zao la korosho ndio linaanza kulimwa katika mkoa huo ni vema wakaweka utaratibu wa kuwapeleka wakulima katika vituo vya utafiti wa kilimo kwa lengo la kuwafanya wakulima hao kulima kwa tija.
Naye, mmiliki wa shamba hilo Karegere aliishukuru Serikali kwa kuwaongezea zao lingine na yeye ni miongoni mwa wakulima walionufaika kwa kupewa miche ya mikorosho bure.






0 comments:
Post a Comment