Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Januari, 2017
ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Mhandisi Felchesmi Mramba.
Kufuatia
kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Tito Esau Mwinuka kuwa
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO.
Kabla ya uteuzi
huo Dkt. Tito Esau Mwinuka alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM). Uteuzi wa Dkt.
Tito Essau Mwinuka unaanza mara moja.
No comments:
Post a Comment