Mkulima
mmoja aitwaye OMARY SULULU mapema Leo tar 1 January 2017 ameshambuliwa
na kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa na panga kichwani na mfugaji kwenye
kijiji cha MAMOYO kata Ya MABWEREBWERE Jimbo La Mikumi. Tukio hilo
limetokea baada ya Ndugu OMARY SULULU alivyokuwa akijaribu kufukuza
mifugo hiyo kwenye mashamba ya Migomba, nyanya na Mahindi, Kwa sasa
Ndugu OMARY SULULU anaendelea na Matibabu katika Hospitali Ya Wilaya Ya
Kilosa.
Juhudi zilizokwishafanywa na Mhe Mbunge ameweza kuwasiliana na Mkuu wa Wilaya Ya Kilosa kwa hatua zaidi
Lakini
pia Mbunge wa jimbo La Mikumi Mhe JOSEPH LEONARD HAULE anaendelea kutoa
wito na kuiomba sana serikali isaidie kutatua migogoro hii
isiyokwisha ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA.
Imetolewa na:~
Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Jimbo La Mikumi
No comments:
Post a Comment