Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Mbogo Futakamba (Katikati kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na
Menejimenti ya DAWASCO, baada yakumaliza kikao cha kumuaga katibu mkuu huyo
(katikati kulia ) ni Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco.
*******************
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Mbogo Futakamba amewataka wafanyakazi wa Shirika la
Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) kufanya kazi kwa
ushirikiano, nidhamu pamoja na kuwa wabunifu katika kazi, ili kufanikisha
utoaji wa huduma bora ya Majisafi na Majitaka katika jiji la Dar es salaam
pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Hayo yalizungumzwa katika
kikao cha pamoja kilichoandaliwa na menejimenti ya Dawasco cha kumuaga Katibu
Mkuu huyo ambaye anamaliza muda wake wa utumishi katika umma kisheria, kikao
ambacho kilichofanyika makao makuu ya
shirika hilo, jijini Dar es Salaam.
“Nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu mzuri ambao umenipa heshima
na kuniondolea aibu katika suala zima la Maji, ninawasihi muendelee kuwa na
nidhamu pamoja na ubunifu katika kazi kwani mimi mwenyewe nilikuwa mbunifu”.
Aidha, ameipongeza Dawasco kwa
kazi nzuri ambayo wamekuwa wakifanya ikiwemo ya kudhibiti upotevu wa Maji kwa
kiwango kikubwa kwa kuzuia mivujo kwa wakati na wizi wa maji katika maeneo
mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na Pwani.
Naye, Afisa Mtendaji mkuu wa
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco), Mhandisi
Cyprian Luhemeja amempongeza katibu mkuu huyo kwa ushirikiano na uaminifu
mkubwa alionyesha kipindi chote cha utumishi wake, amemtakia heri na mafanikio
katika maisha yake mapya anayokwenda kuyaanza.
“Kwa niaba ya wafanyakazi wote, tunakushukuru sana mzee wetu kwa
mchango wako mkubwa katika shirika kipindi chote cha utumishi wako, tumejifunza
mengi kutoka kwako, sisi wafanyakazi wa Dawasco tunakuombea Baraka na mafanikio
makubwa katika maisha yako mapya ya ustaafu”.
No comments:
Post a Comment