Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Diana Masalla akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya semina ya siku moja ya madalali
wa Bima iliyolenga kuwaelimisha kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) katika
Bima.
Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa Bima Tanzania Mohamed
Jaffer akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam baada ya semina
ya siku moja ya madalali wa Bima na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaelimisha kuhusu Kodi ya Ongezeko
la Thamani(VAT) kwa sekta za Bima.
******************
Na Tiganya
Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo ya siku moja kwa
Madalali wa Bima Tanzania yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuifahamu vema
Sheria ya Kodi ya Mwaka 2014 ili waweze kushiriki vema na kuondoa kasoro katika
ulipaji wa Kodi ya ongezeko la Thamani kutoka Sekta ya Bima.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Meneja wa
Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Diana Masalla wakati
wa mkutano waandishi wa habri kwenye semina ya siku moja kwa Madalali wa Bima(
Insurance Brokers) ya kuwajengea uwezo kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT).
Alisema kuwa mafunzo hayo yamewaelimisha wanachama hao juu ya
Kodi ya zuio , utoaji wa kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) na jinsi ya kulipa
kwa njia ya mtandao(Revenue gateway system).
Alisema kuwa TRA imekuwa ikitoa mafunzo hayo kwa Wanachama na
Mawakala wa Bima kwa sababu kabla ya Sheria ya Mwaka 2014 walikuwa halipi Kodi
na hivyo semina hiyo imesaidia wanachama hao kuwa na uelewa mpana juu ya
ulipajji wa kodi ya ongezeko la thamani.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa Bima
Tanzania Mohamed Jaffer aliipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa hatua
yake ya kutoa elimu kwa wanachama wake kwani imesaidia sana kuwajengea uwezo
ambao utasaidia ulipaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani.
Aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuondoa makosa katika
masuala ya ulipajji kodi na jinsi ya ujazaji wa malipo ya kodi kwa wanachama
wao.
Jaffer alisema kuwa ni muhimu sana wanachama wa Chama chake kuelewa
vema jinsi ya kujaza na kulipa kodi kwani asilimia 60 ya mapato ya Bima yanatokana
na madalali wa Bima kwa kuwa wao ndio wako karibu na wateja kuliko Kampuni za
Bima ambazo zinabaki na asilimia 40.
Alisema kuwa hadi hivi Chama hicho kina wanachama wapato 150 ambao
wamesambaa Nchi nzima ambao kwa mwaka uliopita waliweza kukusanya wastani wa
shilingi bilioni 370.
Kati ya fedha hizo asilimia 18 ndio ulipwa kodi ya ongezeko
la thamani na kuongeza kuwa kiwango cha makusanyo kwa mwaka huu kinatarajjiwa
kuongeza na hivyo kuongeza mapato ya kodi ya VAT.
No comments:
Post a Comment