Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza uteuzi wa viongozi ya Tume ya Uchaguzi, Tume ya Maadili na Majaji wa Mahakama ya Rufaa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 22, 2016.
********************
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 22
Desemba, 2016 amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage
kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Jaji
Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka 5
kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Mhe.
Jaji Semistocles Kaijage anachukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ambae
muda wake wa kuwa Mwenyekiti umemalizika rasmi mnamo tarehe 19 Desemba, 2016.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahamoud Hamid kuwa Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kipindi kingine cha miaka 5
kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Mhe.
Jaji Mstaafu Hamid Mahamoud Hamid alikuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC na amemaliza
kipindi chake cha kwanza cha miaka 5 mnamo tarehe 19 Desemba, 2016.
Halikadhalika,
Mhe. Rais Magufuli pia amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji
Harold Reginald Nsekela kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia tarehe 20 Desemba,
2016.
Mhe.
Jaji Mstaafu Nsekela anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Mstaafu
Salome S. Kaganda ambae amestaafu mnamo tarehe 10 Desemba, 2016.
Katika
hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amewateua
Majaji 4 wa Mahakama Kuu kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani kuanzia leo tarehe
22 Desemba, 2016 kama ifuatavyo:-
i) Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika
ii) Mhe. Jaji Jackobs Mwambegele
iii) Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye
iv) Mhe. Jaji Sivangilwe Sikalalilwa Mwangesi
Wateule
wote waliotajwa katika taarifa hii wataapishwa kesho Ijumaa, tarehe 23 Desemba,
2016 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment