December 22, 2016

DCB COMMERCIAL BANK YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KWA SEKTA YA BENKI, NDOGO NA KATI KWA UBORA WA UANDAAJI NA UWASILISHAJI WA TAARIFA ZA HESABU MWAKA 2015.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Edmund Mkwawa akiwa na tuzo waliyoshinda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari juu ya zawadi waliyoipata kwenye sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015.
 Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa  akiwa ambebebelea zawadi waliyoipata ya sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015, pamoja na viongozi wengine wa benki hiyo.
DCB COMMERCIAL BANK YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KWA SEKTA YA BENKI, NDOGO NA KATI KWA UBORA WA UANDAAJI NA UWASILISHAJI WA TAARIFA ZA HESABU MWAKA 2015.

Ndugu Wanahabari,
Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha hapa leo. Lengo la kuwaiteni ni kutoa taarifa kwa umma juu ya DCB Commercial Bank kuwa mshindi wa kwanza kwa sekta za benki, ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa  taarifa za mahesabu mwaka 2015. Hii ni tuzo ambayo inaandaliwa kila mwaka na Bodi ya Uhasibu Tanzania ( NBAA).

Mashindano haya yalianza tangu miaka ya 2011, na katika kipindi chote hicho DCB Commercial bank imeweza kufanya vizuri. Kwa miaka minne mfululizo mwaka 2011 hadi 2014, Benki imeshika nafasi ya 3 miongoni mwa benki za Tanzania kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za Hesabu na kwa mwaka wa 2015, DCB imekuwa mshindi wa kwanza kwa sekta ya benki, ndogo na za kati.  Kwetu sisi ni fahari kubwa na tunajivunia mafanikio tuliyopata ikiwa ni kielelezo kwamba DCB Benki inafuata miongozo ya utawala bora, tunaomba wadau na wawekezaji wetu kuwa na imani juu ya usalama wa fedha zao walizowekeza DCB. Tunawaomba muendelee kuitumia Benki ya DCB kwa shughuli zote za kibenki. Tunaahidi kuendeleza mafanikio haya kwa ustawi wa Benki, wateja, wawekezaji na Taifa kwa ujumla.
 
Ndugu Wanahabari
Mafanikio mengine ambayo benki imepata ni pamoja na:-
·  Kutimiza miaka 14 ya utoaji huduma bora za kibenki kwa Wajasiriamali, mwaka 2017 benki itasheherekea miaka 15 ya utoaji huduma bora kwa wajasirimali.
·   Benki imepata faida  kila mwaka kuanzia mwaka 2006
·   Kulipa gawio kwa wanahisa wa benki kila mwaka
· Kuongezeka kwa matawi kutoka matawi 2 mwaka 2005 hadi matawi 9 mwaka 2016. Mwaka 2017 benki itafungua tawi la 10 makao makuu ya nchi, Dodoma.
·  Kuwa na mtaji imara wa shi. Bilioni 32.
·   Upanuaji na uboreshaji wa huduma za kisasa kwa wateja wetu kupitia Agency Banking (DCB Jirani) ambayo inawawezesha wateja wetu kupata huduma mbalimbali za kibenki kupitia mawakala walioidhinishwa na DCB katika vitongoji, DCB Pesa huduma ambayo inamuwezesha mteja kufanya miamala ya benki kutuma na kupokea pesa kupitia simu ya mkononi, kupata huduma hii si lazima mteja kuwa na akaunti na DCB Benki. Huduma hii ni mpya, pamoja na agency Banking zitazinduliwa rasmi Januari mwakani, leo tumewaita mawakala wetu kuongea nao juu ya kuanza kipindi cha majaribio cha mwezi na baada ya kujiridhisha tutazindua rasmi huduma hizi.

Ndugu Wanahabari
Kwa sasa benki iko kwenye promosheni ya Boresha maisha na DCB, pata faida na DCB ya hadi asilimia 15% kwa kufungua akaunti ya amana za muda maalum.  Tunatoa wito kwa wateja wetu na wasiowateja, mashirika ya umma, wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kufungua akaunti au kuweka pesa kwenye akaunti ili muweze kujipatia zawadi mbalimbali baada ya kushinda bahati nasibu.

Mwisho
Uongozi wa benki unapenda kuwatakia wateja wake na wananchi kwa ujumla sikukuu njema ya Christmas na mwaka mpya 2017.

E.P. MKWAWA
MKURUGENZI MTENDAJI
DCB COMMERCIAL BANK PLC
DISEMBA 2016.

No comments:

Post a Comment