Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, Kanali Marko Gaguti akizungumza na mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Munanila, Wilayani humo katika siku yake ya kwanza ya kutembelea kaya kaya 307 zilizo andikishwakunufaika kupitia mfuko wa TASAF kusaidia kaya masikini.
Kanali Gaguti akiendelea na ziara yake.
Hapa ni kama mhusika hakuwepo nyumbani.
Kanali Gaguti akizungumza na mmoja wa nufaika.
Na Father Kidevu Blog- Buhigwe
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe
Kanali Marko Gaguti ameanza ziara ya siku 10 ya kutembelea nyumba kwa
nyumba ilikuweza kuwabaini watu
wanaonufaika na mpango wa kuwasaidia kaya masikini TASAF awamu ya tatu
ambao hawana sifa ya kunufaika na mpango huo waweze kuondolewa.
Katika ziara hiyo iliyoanza
jana katika Kijiji cha Munanila alisema katika Wilaya ya Buhigwe kuna jumla ya
kaya 307 zilizo andikishwa kama kaya masikini lakini hazina vigezo vya
kunufaika na mradi huu kutokana na hali zao za kiuchumi na mazingira wanayo ishi hayaonyeshi kuwa ni masikini
hivyo watatakiwa kuondolewa katika mpango huo.
Alisema Ziara hiyo itafanyika
kwa siku kumi itahusisha viongozi wote wa ngazi ya Kijiji,kata na Wilaya
ilikuweza kuwabaini wale wote ambao hawastahili nyumba kwa nyumba ili
waondolewe na wanufaika wabaki kuwa wale wanao stahili tuu kupatiwa msaada huo
wa kaya lengwa.
Gaguti alisema kunabaadhi ya
wanufaika wamekimbia baada ya kupewa taarifa ya uhakiki wa wanufaika wa mradi
huo kwa kuhofia wanaweza kutolewa kwa
wale ambao hawakuwepo kwenye kaya zao ilikuweza kuhakikiwa watakuwa
wamejiondoa,kwa sasa tumetoa maelekezo kwa viongozi wa vijiji kushirikiana na
serikali ilikukamilisha suala hilo kwa nakini bila kumpendelea wala kumuonea
mtu yeyote.
"Leo tumeanza zoezi la
kuwabaini wanufaika wasio na sifa zoezi hili litakuwa ni la siku kumi katika
ziara ya leo tumeweza kuwabaini baadhi ya wanufaika hawana sifa watatakiwa
kuondolewa kwenye mradi na kwa waliokwepa kufanyiwa tathimini ya kunufaika na
mradi watakuwa wamejiondoa wenyewe tunahitaji kubaki na watu ambao wanasifa ya
kupatiwa fedha za TASAF ili lengo la serikali la kuzisaidia kaya masikini
litimie",alisema Gaguti.
Kwa upande wake Mratibu wa
TASAF Wilaya ya Buhigwe Chubwa Deogratius alisema mkakati wa kuwaingiza
wahusika ulishirikisha jamii husika pamoja na wenyeviti wa vijiji ambapo
Wananchi wenyewe walikuwa wakidangsnya taarifa yupi anastahili kuingizwa kwenye
mpango na yupi hastahili .
Alisema baada ya kupokea barua
kutoka Wizarali sisi kama wasimamizi wa mpango huu tumeamua kupita nyumba kwa
nyumba kwa walengwa ilikuweza kujilizisha yupi anastahili kuendelea kuingizwa
kwenye mpango na yupi hastahili ilikuweza kukamilisha adhima ya serikali ya
kuzisaidia kaya masikini.
Katika ziara ya siku ya leo
kuna jumla ya kaya tatu ambazo hazina sifa. Anjelina Josia na Veronica James ni
baadhi ya wanufaika walio kuwa kwenye
mpango na hawana vigezo vya kuwemo kwenye mpango huo wakati kuna baadhi wenye
vigezo vya kuwa kaya masikini wameshindwa kuingizwa kwenye mpango hali ambayo
inatia wasiwasi na ziara hiyo kuendelea
na uchunguzi.
No comments:
Post a Comment