Meneja Mwandamizi Mikakati na Ubunifu wa Benki ya DCB,
Samwel Dyamo (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar
es Salaam jana wakati Benki hioyo ikitangaza promotion maalum kwa wateja wapya
na wazamani wa benki hiyo Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa
Shughuli za kibenki, Haika Machaku na kushoto ni Meneja Masoko wa Benki ya DCB,
Boyd Mwaisame.
Meneja Mwandamizi Mikakati na Ubunifu wa Benki ya DCB,
Samwel Dyamo (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar
es Salaam jana wakati Benki hioyo ikitangaza promotion maalum kwa wateja wapya
na wazamani wa benki hiyo Dar es Salaam jana
***************
TAARIFA
KWA WAANDISHI WA HABARI JUU YA KAMPENI YA KUWEKA AMANA DCB BENKI INAYOITWA
‘BORESHA MAISHA NA DCB, PATA FAIDA NA DCB’
DCB Commercial Bank, iliyo anza kutoa
huduma kwa wateja miaka 14 iliyopita sasa inawaletea wateja wake kampeni maalum
inayoitwa ‘Boresha Maisha na DCB, Pata Faida na DCB’ kwa kipindi cha miezi mitatu
kuanzia Novemba 28 mwaka huu hadi 29 Februari 2017.
Kampeni ya Boresha maisha na DCB
inalenga kunufaisha kwa kutoa zawadi kwa wateja wetu wapya na wa zamani, baada
ya kuweka pesa mara kwa mara kwenye akaunti mojawapo ya Akiba binafsi, akaunti
ya watoto na akaunti ya WAHI kiasi cha kuanzia shi. 50,000 na kuendelea na
kuongeza amana kwenye akaunti zao mara mbili zaidi ya Shi. 500,000. Mteja huyu
atapata nafasi ya kuingia kwenye draw ya bahati nasibu itakayochezeshwa kila
mwezi na kujishindia Tshirt, simu za mkononi au pesa taslimu shi. 200,000 kwa
ajili ya ada ya mtoto shule.
Tunatarajia kuchezesha draw tatu za bahati nasibu,
draw ya kwanza itachezwa tarehe 17 Disemba 2016, ya pili tarehe 17 Januari 2017
na ya mwisho itachezwa tarehe 17 Februari 2017. Washindi watataarifiwa mara
moja baada ya kushinda mbele ya waandishi wa habari na ili kuwatambua
watatakiwa kuwasilisha vitambulisho vyao wakati wa kuchukua zawadi zao mojawapo
ya vifuatavyo; leseni ya udereva, kitambulisho cha mpiga kura au kitambulisha
cha utaifa.
Idadi ya washindi kwa kila draw ya bahati nasibu itakuwa kama ifuatavyo:
i.
Washindi
wa Tshirts watakuwa - 20
ii.
Washindi
wa simu za mkononi - 2
iii.
Washindi
wa pesa taslimum kwa ajili ya ada shule - 3.
Pata faida na DCB ni kampeni
inayowapa faida kubwa wateja wetu kwa kuwekeza na DCB kupitia huduma yetu ya
Akaunti ya muda maalumu. Kwa wateja wetu watakao wekeza DCB kiasi cha shi.
Milioni 50 na kuendelea kwa muda wa kuanzia mwaka mmoja watapata faida kubwa ya
hadi asilimia 15 na kuendelea kutegemeana na Ukubwa wa amana zake.
Tunatoa wito kwa wateja wetu na wasio
wateja, watu binafsi, wajasiriamali na
taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano hili na kufaidika.
Kadhalika tunawashukuru sana wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma bora
kutoka DCB Commecial Bank. Tunawaahidi tutaendelea kuboresha zaidi huduma zetu
ili muendelee kufaidika nazo kupitia kampeni hii ya Boresha maisha na DCB, Faidika
na DCB.
No comments:
Post a Comment