Madiwani wakiwa kwenye kikao.
Na Farher Kidevu Blog, Kigoma
MADIWANI wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia vikao vya kamati limeadhimia kuwasimamisha kazi watumishi wawili ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa takribani milioni 42 pamoja na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo kiasi cha shilingi milioni 250.
Maamuzi hayo yalichukuliwa mara baada ya kamati mbalimbali kujiridhisha na upotevu wa fedha kiasi cha milioni 42 ambazo zilihamishwa kutoka akaunti ya Amana na kupelekwa kwenye akaunti ya maendeleo na kutumiwa kulipa miradi mingine ya maendeleo iliyokuwa ikisimamiwa na Manispaa hiyo lakini pia matumizi mabaya ya fedha kiasi cha shilingi milioni 250 ambapo tume imeundwa ili kuchunguza zaidi tuhuma hizo.
Akitoa ufafanuzi Meya wa Manispaa hiyo Hussen Ruhava akizungumza mara baada ya maamuzi hayo alisema tume imeundwa kuchunguza watumishi wanne kati ya sita wamechukuliwa hatua za kinidhamu na kuwajibika kulipa fedha hizo huku kati ya hao wawili wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi na hatua za kisheria zitachukuliwa.
Ruhava aliiwataja walio simamishwa kuwa ni Christina Nayingu Ambae ni muhasibu wa Manispaa na Michael muhadhini wa Ndoliwa muhadhina wasultani Ndoliwa na DrJohni Tratra kuwa watasimamishwa ilikupisha uchunguzi pindi utakapo kamilika watatakiwa kulipa kiasi chote cha fedha kilicho tolewa.
Aidha Ruhava alisema licha ya maamuzi hayo lakini pia wameeleza kutokuwa na imani na mkurugenzi wa Manispaa Judethadeus Mboya kutokana na kushindwa kukusanya mapato ipasavyo, asilimia kumi kutotolewa kwa vijana na wanawake, sanjari na asilimia 20 ya maendeleo kutokufika katika maeneo husika lakini pia sakata hilo lilimkumba na afisa mipango miji kushindwa kutekeleza maamuzi ya vikao vya madiwani na hivyo kuchukuliwa hatua zakinidhamu.
" hatutaki kufanya maamuzi ya kumuone mtu hatutaki kuchukua maamuzi ya kuwa karibisha watu tunacho hitaji watumishi wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi bira ubadhirifu wowote na kutenda haki ",alisema Ruhava
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Rusimbi Butije Butije ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Mipango miji alisema chanzo cha kuwasimamisha watumishi hao ni kuhofia kuwa fedha hizo za miradi kutoka na kuto kushirikishwa kwa kamati ya fedha na mipango ambapo ni lazima kabla fedha za moradi ya maendeleo kutolewa kamati hizo zishirikishwe.
Alisema Baadhi ya watumishi wamesimamishwa na wengine wataendelea na kazi wakati uchunguzi unaendelea endapo watagundelika hatua za kinidhamu zitachukuliwa mapema iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment