Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mikoa na Utawala Bw. Raymond Mndolwa akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga wakati alipoelezea madeni yaliyolipwa na wadaiwa sugu na ambayo yanaendelea kulipwa , Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawaliano NHC Bi Susan Omari.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mikoa na Utawala Bw. Raymond Mndolwa akizizitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga wakati alipoelezea madeni yaliyolipwa na wadaiwa sugu na ambayo yanaendelea kulipwa , Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawaliano NHC Bi Susan Omari.
Baadhi ya waandishiwa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mikoa na Utawala Bw. Raymond Mndolwa.
.......................................................................................
Shirika la Nyumba la Taifa lilitoa taarifa ya madeni ya idara na taasisi mbalimbali za serikali pamoja na watu binafsi mwezi Septemba 2016. Deni lililokuwa linadaiwa ni kama ifuatavyo:
- Serikali Shs 9,346,682,763.63
- Watu binafsi Shs 2,569,446,334.64 na dola za kimarekani 380,933.62
Baada ya agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Shirika lilitoa notisi kwa taasisi zote za serikali na watu binafsi kulipa malimbikizo yao ndani ya siku saba (7) ambazo Mhe. Rais aliagiza.
Jumla ya shilingi 5,981,320,179.15 zimelipwa na taasisi mbalimbali za serikali zilizokuwa zinadaiwa na deni lililobaki la shilingi 3,365,362,584.48 limeendelea kufuatiliwa na tu tunaamini idara na taasisi husika zitamaliza deni lake ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba 2016. Ni vizuri pia ikaeleweka kuwa ni sehemu kidogo ya idara na taasisi za serikali ambazo zimepanga katika majengo yetu.
Tunatoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais kwani kwa mara ya kwanza serikali na taasisi zake zilizokuwa zinadaiwa ziliweza kutekeleza agizo hilo kwa kiwango kikubwa sana. Tunampongeza sana Mhe. Rais kwa msukumo wa kuliunga mkono Shirika la Nyumba la Taifa katika jitihada zake za kuboresha makazi ya Watanzania.
Ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais za kuhamishia ya nchi mkoani Dodoma, Shirika limeelekeza fedha zote zilizokusanywa kwenye madeni kuanza ujenzi wa nyumba 300 za makazi kwenye eneo la Iyumbu pembeni mwa Jengo la Utawala la Chuo Kikuu cha Dodoma na ujenzi huo umekwishaanza.
Pamoja na watu binafsi kulipa, wapo ambao wameendelea kulimbikiza madeni. Tunawataarifu wapangaji binafsi wa makazi na biashara kwamba zoezi kabambe la kuwaondoa wote wanaodaiwa limekwishaanza na yoyote mwenye deni yafuatayo yatatekelezwa:
- Kuwaondoa kwenye majengo ya Shirika na kuuza samani zao kufidia deni linalodaiwa;
- Kuwatoa kwenye vyombo vya habari ikiwemo magazeti; na
- Kuwapeleka mahakamani ili ikibidi njia nyingine za kisheria zitumike kilipa deni la Shirika.
Tunapende kuwahimiza wapangaji wetu watimize wajibu wao ili kuepuka usumbufu hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
No comments:
Post a Comment