Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya gari na
ndege ya kuchezea Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo huku Mama yake Jumanne
akishuhudia.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem
Al Najem akimkabidhi zawadi ya dawa Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi ambazo zitatumika
kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto Prof. Ayoub Magimba na Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge.
Balozi wa Kuwait
Nchini Mhe. Jasem
Al Najem akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam ili kuona ni jinsi gani nchi yake itakavyoisaidia
Taasisi hiyo. Kulia kwa Balozi ni Mkurugenzi
Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi.
Daktari Bingwa
wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuelezea takwimu za upasuaji
wa wagonjwa wa Moyo zinazofanywa na Taasisi hiyo Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem
Al Najem (kushoto). Wapili kulia ni Dkt. Barjces Almutairi kutoka Mfuko wa
Kusaidia wagonjwa wa nchini Kuwait akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo Tulizo Shemu Sanga.
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya gari na
ndege ya kuchezea Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo huku Mama yake Jumanne
akishuhudia.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem
Al Najem akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati balozi huyo
alipotembelea Taasisi hiyo na kuahidi kuisaidia vifaa vya kutunzia damu na
kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji wa moyo katika chumba cha upasuaji. Kulia
ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter
Kisenge.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem
Al Najem akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete na Ubalozi wa Kuwait mara baada ya kumalizika kwa ziara yake aliyoifanya
katika Taasisi hiyo. Kulia kwa Mhe. Balozi ni Mkurugenzi
Mtendaji JKCI Prof. Mohamed Janabi.
No comments:
Post a Comment