November 30, 2016

MADIWANI MERU WAMKATAA MKURUGENZI

 Makamu mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Meru akiwa anachangia hoja katika baraza hilo
 baadhi ya madiwani wa meru wakifuatilia kikao
 Mkurugenzi   wa halmashauri ya Meru  Christopher Kazer akifafanua jambo kwa waandishi mara baada ya baraza kumalizika
  mkurugenzi   wa halmashauri ya Meru  Christopher Kazer akijibu hoja mbele ya madiwani wa meru
 baadhi ya madiwani wakifuatailia

 Habari picha na  Woinde Shizza,Arusha
BARAZA la madiwani  Halmashauri ya Meru mkoani Arusha wamkaanga Mkurugenzi wasema hana uwezo wa kuongoza  Halmashauri hiyo.

Akitoa  maazimio  ya kikao  cha baraza kilichokaa siku mbili kilichowajumuisha  madiwani,wakuu wa idara mbalimbali na wataalam Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Willy Njau Alisema wametafakari kwa kina utendaji wa Mkurugenzi na kubaini kuwa hafai.

" Tumejadili ajenda ya utendaji  usioridhisha wa Mkurugenzi wetu na tumeona  kuwa haufai kutokana na mambo mengi anayoyafanya yanakiuka kanuni na taratibu za Halmashauri"alisema Njau.

Aidha Njau alisema Mkurugenzi huyo ameonekana kukata mawasiliano na mwenyekiti wa Halmashauri jambo alilosema siyo sahihi.

Alisema pia ameweza kukata mawasiliano na madiwani wa Halmashauri hiyo pamoja na kusababisha hata wakuu wa idara kutokuwa na mawasiliano na madiwani jambo linalorudisha maendeleo nyuma.

Aliongeza kuwa Mkurugenzi huyo ameshindwa kukusanya makusanyo ya pesa kiasi cha milioni 150 kilichokusudiwa kukusanywa  tangu  Julai hadi septemba mwaka huu jambo alilosema linaweza kusababisha Halmashauri kutopewa ruzuku kutoka serikali kwasababu  ya uzembe.

" Tumejiridhisha kuwa uwezo wa Mkurugenzi kuiongoza Halmashauri yetu kama Mkurugenzi Mtendaji ni mdogo hivyo hafai anadidimiza maendeleo ya Halmashauri ya meru" alisema Njau. Na kuongeza.

"Tumeamua kuiomba mamlaka yake  na Uteuzi ichukue  hatua stahiki za kumuwajibisha ili kunusuru maendeleo ya Halmashauri ya meru"

Vilevile alisema  kuwa  Mkurugenzi huyo amekuwa  akidharau maagizo yanayotolewa na  kamati mbalimbali za baraza hilo na Kushindwa kuzitekeleza ambapo ni kuvunja kanuni na taratibu za Halmashauri.

Hata hivyo alisema kitendo cha mkurugenzi kukata posho zamadiwani ni kinyume na utaratibu kwani ziliwekwa kisheria ambapo alisema  Kama kuna tatizo la kukatwa  posho ni lazima sheria hiyo ingebadilishwa kwanza.

" Mwenye dhamana ya kutangaza kuwa posho zinabadilika ni Waziri mwenye dhamana hiyo  lakini siyo mkuu wa mkoa, Wilaya au Mkurugenzi" alisema .
Naye Diwani wa Kikatiti  Elisa Mungure ambaye ni Mwenyekiti wa madiwani alisema Mkurugenzi huyo amekuwa  akiendesha Halmashauri kisiasa jambo ambalo halifai.

" Ninasikitishwa na uongo unaoelezwa na Mkurugenzi ambaye kateuliwa na mheshimiwa Rais hii ni ajabu haiwezekani kuendelea kumuamini mtu wa aina hii" alisema Mungure.

Alisema Mkurugenzi huyo amekuwa  akiwqhamisha watendaji wa kata  bila  kufuata taratibu huku akishinikiza ofisi ya kata ya Kikatiti kuwa ni ya CCM  huku ikiwa ni ofisi ya wananchi wala siyo ya chama chochote.

Kwa upande wake mkurugenzi  Huyo Christopher Kazer  alisema anafuata maagizo ya mkuu wa nchi na hawezi kuwanyima watu kufikiri  wanavyofikiri.

" Maelekezo ya kupunguza matumizi yasiyolazima kutoka kwa mkuu wa nchi ninayafuata pia ndio maana nimepunguza matumizi mengi" alisema.

Alisema hawezi kuzuia maamuzi yanayotolewa na baraza hilo maana kwa namna moja au nyingine wamekaa wakatengeneza maamuzi hivyo hawezi kuwalazimisha kutofanya maamuzi.

Aidha pia alibainisha kuwa anaamini kabisa madiwani hawa wanataka halmashauri iendeshe kisiasa wanataka iendeshwe kama wao wanavyotaka kitu ambacho hatakubali kwani sio hakutumwa kufanya kazi ya siasa bali alitumwa kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi na serikali kwa ujumla 

Alisema kuwa anaamini haya yote yanatokea kutokana na madiwani hawa kukatwa fedha za posho na usafiri ambao walikuwa wamejiwekea bila kufuata taratibu

"ivi jamani ndugu waandishi mtu anatoka apo usa anataka alipwe nauli elfu 80 ni haki kweli wengine wanatoka apa apa wakija kikao kikichelewa kuisha wanataka walipwe  fedha za kulala laki laki sasa mimi hayo yote tumeyatoa sasa ivi wanalipwa elfu 40 tu na mshahara wao upo pale pale sasa wao ndio maana wananipiga zwegwe mimi nasema nitasimamia ilani ya chama ambacho kinaongoza serikali pia nitafata sera ya muheshimiwa Rais ya kubana matumizi sitakubali  wafanye vitu ovyo na ninyamaze walifikia atua wakataka hata kunigombanisha na watendaji wangu ila mimi nimeajiriwa na serikali mimi sio mwanasiasa na nitafanya kazi kama nilivyoaaidi siku nilioapishwa "alisema mkurugenzi  Kazer

No comments:

Post a Comment