October 24, 2016

WATANGAZAJI WA LAKE FM MWANZA KUTAMBULISHWA KWA WANANZENGO KWENYE USIKU WA MSHIKE MSHIKE NA KHADIJA KOPA

Usisahau kuhusu Show ya Usiku wa Mshike Mshike na Mfalme wa taarabu Afrka Mashariki na Kati iliyoandaliwa na 102.5 Lake Fm Mwanza.

Ni alhamisi wiki hii tarehe 27.10.2016 ndani ya kiwanja cha nyumbani, Villa Park Resort, kwa kiingilio cha shilingi 7,000 kabla ya saa tano usiku na shilingi 10,000 baada ya saa tano usiku.

Pia watatambulishwa watangazaji wa Lake Fm wakiongozwa na Aisha BBM anayetangaza kipindi cha Mshike Mshike jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa saba mchana, Ma'Djz wa Lake Fm pamoja na wananzengo wengine wanaoendelea kuhakikisha redio hiyo inazidi kupenya Jijini Mwanza.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi
Malikia wa taarabu Afrika Mashariki na Kati, Khadija Kopa.

No comments:

Post a Comment