Kampuni ya Maxcom Africa Leo imezindua rasmi mfumo mpya unaowezesha watumiaji wa huduma za bima kufanikisha huduma kwa njia ya Mtandao. Huduma hii ya kipekee unawawezesha wateja wa kufanya makadirio na Malipo ya bima kwa Njia ya mtandao ambayo ni teknolojia ya kisasa Zaidi kwenye utoaji wa huduma za Bima.
Akielezea Huduma hii Meneja wa ukuzaji wa Biashara Bw. Tony Misokiye anaelezea kwamba kutokana na changamoto mbalimbali ambazo walipabima wanakumbana nazo ikiwamo changamoto ya kufikia ofisi za bima, changamoto ya kupata Huduma kwa wakati na Pia uhakiki wa malipo ya bima.
Maxcom Africa Imetengeneza mfumo madhubuti ambao mlipa bima anaweza kutathmini kiasi cha malipo ya bima ya chombo chake cha usafiri kwa njia ya Mtandao kisha kulipia kwa mitandao ya simu au Visa Mastercard, akifafanua Zaidi bwana Misokiye amesema, ni teknolojia ya kipekee hapa Tanzania na Africa kwa ujumla kwani malipo ya bima huifikia kampuni husika papo hapo.
Meneja Ukuzaji wa Biashara ya Bima wa Kampuni ya Maxcom Africa Bw. Tony Misokiye Akiuelezea Mfumo huu Ulio zinduliwa mwishoni mwa wiki kwa wadau walioshiriki.
Akielezea Jinsi ya Kufanya bwana Misokiye amesema ili kukadiria thamani na kiasi cha bima, Mlipaji anatakiwa kuingia kwenye www.insurance.maxmalipo.com kisha ajisajili na kuanza kutathmini gharama za malipo ya Bima. Mfumo huu pia unakipengeke kinachowawezesha Mawakala na makampuni ya bima kujisajili na kupokea malipo yao kwa Njia ya Mtandao.
Pamoja na hayo pia upatikanaji wa ticker kwa mtumiaji unasimamiwa na Wakala au kampuni husika ya bima kutokana na chaguo la Mteja, Pia Misokiye ameeleza kwamba baada ya Malipo kabla ya kupata stika husika mteja anapatiwa uthibitisho wa Malipo.
Naye Mkurugenzi wa Uwendeshaji wa Kampuni hii ya Maxcom Africa (Group Chief Operations Officer) Bwana Jameson Kassati ameeleza kwamba Kampuni ya Maxcom Africa imekua ikijikita kwenye kuhakikisha kwamba inafanikisha adhma yake ya kuisaidia Jamii kuzifikia huduma mbalimbali kwa urahisi na kwa usalama zaidi.
Akisema “ Leo hii tumeingia kwenye huduma ya Bima tukitambua umuhimu wa bima kwa mtumiaji yeyote wa chombo cha usafiri, na pia tukifahamu changamoto wanazozipata mawakala na makampuni ya Bima hasa kuwafikia watanzania walio wengi”.
Maxcom Imeendele kuwa na ubunifu wa hali ya juu na kuingia kwenye nchi mbali mbali za Africa ikiwamo Rwanda,Burundi na Uganda. Bwana Kassati ametoa wito kwa watumiaji wa Bima kutumia Mfumo Huu kwani ni mfumo salama na wakisasa zaidi kwenye kufanikisha malipo ya Bima hapa Tanzania, pia makampuni ya Bima na mawakala wamehimizwa kujisajili kwenye huu mfumo ili waweze kupokea malipo yao ya bima kwa Urahisi Zaidi.
Maxcom Africa wamekua vinara wa kusimamia na kuchakata miamala Tanzania mfano; Miamala ya mradi wa Mwendo kasi, TRA Magari, Luku, usafiri wa Majini na kwenye mifumo ya Hospitali.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakibadilishana Mawazo katika uzinduzi huu
|
Baadhi ya watendaji wa Maxmalipo wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mgeni (wa pili kushoto) katika hafla hiyo. |
|
Mkurugenzi Uendeshaji Kanda ya Africa Maxcom Africa, Jameson Kassati (kulia) akiwabadilishana mawazo na baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mfumo huo.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
|
|
Meneja Uendeshaji wa Maxcom Malipo, Jameson Kassati akibadilishana mawazo na Afisa Mwandamizi wa Uhasibu wa Kampuni ya ARIS, Salome Kaluzi. |
Meneja Ukuzaji wa Biashara wa Kampuni ya Maxcom Africa Nana Makaya (Kulia) Akibadilishana Mawazo na Moja ya Wageni waalikwa kutoka Tigo
|
Baadhi ya Wageni Waalikwa Wakijadili Mfumo huu |
Mkuu wa Kitengo cha Ubunifu na Ukuzaji biashara Maxcom Africa Bwana Magesa Wandwi (Kulia) Akibadilishana mawazo na moja ya wageni walioshiriki Uzinduzi huu
|
Baadhi wa wageni waalikwa Wakipata Ufafanuzi baada ya Mfumo huu kutoka Kwa Moja ya Mameneja wa Ukuzaji biashara Bw. Tony Misokiye |
|
Baadhi ya Wadau Wakibadilishana Mawazo |
|
Mkurugenzi wa Uendeshaji Kanda ya Africa Maxcom Africa - Maxmalipo, Jameson Kassati (kulia) akiwabadilishana mawazo na mmoja wa wageni katika hafla hiyo. |
|
Mkurugenzi Uendeshaji wa Maxcom Africa Kanda ya Africa, Jameson Kassati (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamaoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na baadhi ya wadau wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. (Imeandaliwa na Robert Okanda blogspot) |
No comments:
Post a Comment