Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akiongea na Waandishi wa
vyombo vya habari juu umuhimu wa uwekaji wa akiba duniani. Kulia ni Meneja
Masoko wa TPB, Grace Majige na Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki, Timotheo
Mwakifulefule.
Mteja
wa TPB tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akiongea na Waandishi wa vyombo vya
habari juu ya faida alizozipata kutoka na kuweka akiba katika benki hiyo.
Kushoto kwake niMeneja wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya na Afisa
Uhusiano na Mawasiliano ya Benki, Timotheo Mwakifulefule (kulia)
Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja
ya wateja wa tawi hilo Alex Lwamanya katika uzinduzi wa mwezi wa akiba duniani.
Kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki, Timotheo Mwakifulefule
Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja
ya wateja wa tawi hilo Grace Mgala katika uzinduzi wa mwezi wa akiba duniani. Kushoto
ni Afisa Mwandamizi wa huduma kwa wateja, Glory Mutta.
Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja
ya wateja wa tawi hilo Mohammed Salim katika uzinduzi wa
mwezi wa akiba duniani.
Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja
ya wateja wa tawi hilo Jumanne Waziri katika uzinduzi wa mwezi wa akiba
duniani. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BENKI ya Posta nchini (TPB) imezindua mwezi
wa uwekaji akiba duniani inayokwenda sambamba na kampeni iliyopewa jina la
“Asante Mteja”.
Akizungumza Jijini
Dar es Salaam jana katika uzinduzi huo, Meneja wa benki ya TPB tawi la
Kariakoo, Patrick Swenya alisema kuwa kampeni hiyo itaendeshwa nchi nzima
katika matawi yao. Alisema, lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha wateja wa TPB
kuweka akiba ili kuweza kufanikisha malengo yao katika maisha ikiwemo ulipaji
wa ada za wanafunzi.
Meneja huyo alisema kuwa katika kuhakikisha wateja
wao wanafanikiwa watatoka na kutembelea wateja wao ambao wengi ni
wafanyabiashara ili kupata mrejesho wa huduma wanazozitoa ikiwemo mikopo kama
imeweza kuwakomboa.
Alisema, kama
watabaini mikopo inayotolewa imewanufaisha watu wengi basi watahakikisha
inaboreshwa zaidi ili kuwakwamua watu wengi kiuchumi. "Katika wiki hii ya
uwekaji akiba duniani tutahakikisha sisi kama TPB tunaboresha huduma zetu ili
kufanikisha zaidi Watanzania ikiwa pia ni moja ya njia ya kuwashukuru kwa
kuchagua Benki yetu", alisema Swenya. Aidha aliongeza kuwa TPB itaendelea
kuboresha huduma ikiwemo mikopo ya vikundi visivyo rasmi inayotolewa kwa riba
nafuu.
Kwa upande wake
mmoja wa wateja wa benki hiyo Alex Lwamanya alisema kuwa mikopo ya riba nafuu
inayotolewa na benki hiyo imeweza kumkwamua kiuchumi kwa kiasi kikubwa.
Alisema, hadi sasa
mikopo hiyo imemuwezesha kujenga nyumba pamoja na kuendeleza biashara zake.
"Nashkuru mikopo niliyoipata na ninayoendelea kupata imenikwamua kimaisha
kwa kiasi kikubwa sana kwani hadi sasa nimeweza kumiliki vitega uchumi
vinavyoniingizia kipato", alisema Alex.
No comments:
Post a Comment