Na Shamimu Nyaki WHUSM.
Serikali imesema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma ya Habari unatoa
fursa kwa wanahabari mbalimbali kuwa na Haki ya kupata Bima ya Afya kwa ajili
ya kupata matibabu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji wa
Serikali Hassan Abbas alipokuwa
akizungumza katika kituo cha Redio E Fm kilichopo Jijini Dar es
Salaam, ambapo ameeleza kuwa Muswada huu utatoa fursa kwa wanahabari kupata
Bima ya Afya na kuondokana na changamoto
ya ukosefu wa fedha ya matibabu .
“Muswada huu utasaidia wanahabari
kuwa na Bima ya Afya itakayosaidia kupata huduma ya kiafya na kuacha
utaratibu ulipo sasa wa kutoa michango wakati mwanahabari anapokuwa mgonjwa au anapofariki.”
Alisema Abbas.
Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa
Sehemu ya tatu ya Muswada huu unaeleza
kuwa kutakuwa na Mfuko kwa ajili ya
Habari ambao lengo lake kuu ni kuwezesha mafunzo kwa wanataaluma ya habari
pamoja na kukuza na kuendeleza utafiti na maendeleo katika nyanja ya Habari na
Mawasiliano ya Umma.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo ametoa rai kwa wadau na
wanatasnia kwa ujumla kuusoma Muswada
huu na kutoa maoni yao ambayo yatasaidia
kuuboresha ili uweze kutumika kwa ajili ya maendeleo ya Tasnia ya Habari.
“Naomba wadau muusome Muswada huu muuelewe na muweze kutoa maoni yenu
kabla haujapelekwa Bungeni kwa mara ya pili ili tasnia hii iwe na hadhi kama
inavyostahili.” Aliongeza Abbas.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 upo katika hatua ya
kujadiliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na
wadau kutoa maoni kwa ajili ya kuuboresha Muswada huo kabla ya kuwasilishwa
Bungeni kujadiliwa.
No comments:
Post a Comment