Mkuu wa wilaya kakokonko Kanali Hosea Ndagala akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka Benki ya NMB na kukabidhiwa na Meneja wa NMB Kakonko Leonard Ngaya. wanaoshuihudia ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kankonko, Dk
Tuluba (kulia) na Mkurugenzi wa Halamashauri
ya Wilaya hiyo, Mwakabibi Lusubilo.
Mkuu wa wilaya kakokonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza katika hafla hiyo ya kupokea msaada wa vifaa tiba kutoka Benki ya NMB. Wengine pichani ni kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kankonko, Dk Tuluba, Meneja wa NMB Kakonko Leonard Ngaya, Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya hiyo, Mwakabibi Lusubilo na Ofisa huduma kwa Wateja wa NMB, Malima Mumanga.
Meneja wa NMB Kakonko Leonard Ngaya akizungumza. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, kanali Hosea Ndagala na kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya.
******************
BENKI ya NMB imekabidhi msaada
wa vitanda na magodoro kwa ajili ya wodi ya wazazi vyote vikiwa na thamani ya
Shilingi Milioni Tano katika kituo cha Afya Mganza Wilayani Kakonko mkoani
Kigoma ambacho kinatumika kama hospitali ya Wilaya.
Msaada huo umekabidhiwa leo na
Meneja wa NMB tawi la kakonko, Leonard Ngaya kwa niaba ya Meneja NMB Kanda ya
Magharibi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala katika hafla fupi
iliyofanyika katika eneo la kituo cha Afya cha Mganza Kakonko.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo Ngaya alisema benki ya NMB imetoa msaada huo kufuatia
maombi yaliyotolewa na Halmashuri hiyo kutokana na upungufu wa vitanda na magodoro katika kituo
hicho cha afya.
Kwa mujibu ya maelezo ya Ngaya
benki hiyo imekuwa ikisaidia msaada miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye jamii katika sekta ya Elimu,afya na
majanga yanapojitokeza ikiwa ni kurudisha sehemu ya faida wanayopata Kwa
jamii ambayo ndiyo wateja wa sekta hiyo.
Aidha hii ni mara ya pili kwa
benki hiyo kutoa msaada wa aina hiyo na aliahidi kuwa NMB itaendelea kutoa
msaada zaidi katika wilaya hiyo pale itakapoombwa kufanya hivyo.
Mkuu wa wilaya wa Kakonko Kanali Hosea Ndagala mara baada ya
kuupokea msaada huo alisema kuwa msaada huo umekuja katika wakati muafaka kwa
kuwa utasaidia kuondoa tatizo la upungufu wa vitanda na magodoro uliyopo katika
kituo hicho cha afya.
Kanali Ndagala ameutaka
uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vifaa hivyo na vingine vinatunzwa ili
viendelee kutoa huduma na kusaidia wananchi wa Kakonko na mewataka kuboresha
huduma ili kupunguza vifo vya akinamama na mtoto.
Ndagala ametoa rai kwa wadau wengine kuiga
mfano wa benki hiyo ya kuchangia katika shughuli za kijamii zinazoikabili
wilaya hiyo.
Mganga mKuu wa kituo hicho Muganza alisema msaada huu wa benki ya nmb
utasaidia kupunguza zaidi vifo vya akinamama wajawazito kujifungulia katika
mazingira mazuri na kuondoa tattizo la wagonjwa kulala wawili wawili.
No comments:
Post a Comment