ISO 9001:2008 CERTIFIED
MASHARTI
YA LESENI KWA WAZALISHAJI WA BIDHAA ZINAZOTOZWA
USHURU
WA BIDHAA (EXCISE GOODS)
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda
kuutaarifu umma kuwa, kwa mujibu wa vifungu vya 8 na 16 vya Sheria ya Ushuru wa
Bidhaa Sura ya 147, wazalishaji wote wa bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa na
wazalishaji wa malighafi ya kutengenezea spiriti wanatakiwa kusajiliwa na
kupewa leseni na Kamishna Mkuu wa TRA kabla ya kuanza uzalishaji. Bidhaa
zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa zimeainishwa katika jedwali la nne la Sheria
husika. Baadhi ya bidhaa hizo ni kama Bia, Sigara, Spiriti, Mvinyo na Vinywaji
baridi.
Masharti ya Leseni
1) Maombi
yote yatumwe kwa Kamishna Mkuu kwa kutumia fomu ya maombi ya leseni
inayopatikana katika ofisi za TRA au tovuti: www.tra.go.tz
2) Maombi
tofauti yafanywe kama ifuatavyo:
a) Kwa
kila kiwanda ambacho kitatumika kuzalisha bidhaa. Leseni itatumika kwa kiwanda kilichopewa
leseni pekee
b) Kwa
kila aina ya bidhaa itakayozalishwa na leseni itatumika kuzalisha bidhaa husika
pekee.
3) Mmiliki
wa leseni hataruhusiwa kuhamisha umiliki wa leseni husika, kubadili kiwanda au
kuzalisha bidhaa tofauti katika kiwanda kilichopewa leseni bila kufanya maombi
na kuruhusiwa na Kamishna Mkuu.
4) Baada
ya kupewa leseni, mzalishaji anatakiwa kumjulisha Kamishna Mkuu juu ya tarehe
ya kuanza uzalishaji ndani ya siku 21 tangu uzalishaji huo kuanza.
5) Pindi
bidhaa yoyote inapoamuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge kuanza kutozwa Ushuru
wa Bidhaa, mzalishaji wake anapaswa kumjulisha Kamishna Mkuu na kuomba leseni
ya uzalishaji ndani ya siku 21 baada ya bidhaa husika kuanza kutozwa Ushuru wa
Bidhaa.
6) Leseni
ya uzalishaji itakwisha muda wake kila tarehe 31 Disemba ya mwaka ambapo
mmiliki atatakiwa kuomba leseni mpya.
7) Wazalishaji
wa spiriti yenye vionjo na isiyo na vionjo (Denatured and Undenatured Spirit)
pia wanatakiwa kuomba leseni za uzalishaji kwa Kamishna Mkuu.
Uzalishaji wa bidhaa zinazotozwa Ushuru
wa Bidhaa bila ya leseni ni kosa linalopelekea adhabu ya faini au kifungo au
faini na kifungo ikiwa ni pamoja na kutaifishwa kwa mitambo na bidhaa zote
zilizohusika katika utendaji wa kosa hili. Wazalishaji wote wanaaswa kumiliki
leseni halali katika wakati wote wa uzalishaji na TRA kwa kushirikiana na wadau
wengine wataendesha ukaguzi endelevu kuhakiki matakwa haya ya sheria.
Waombaji wanatakiwa kufanya maombi katika ofisi yoyote ya
TRA ambako viwanda husika vinapatikana ili kuepuka adhabu kali zinazotokana na
ukiukwaji wa matakwa haya ya sheria.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Limetolewa
na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao Makuu
Dar
es Salaam
No comments:
Post a Comment