Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC)
Beng’i Issa
******
Na Ally Daud-MAELEZO.
WATANZANIA
zaidi ya asilimia 70 wamepewa kipaumbele kushiriki katika shughuli za kujenga uchumi wa
nchi kufikia uchumi wa kati katika kutekeleza sera ya uwezeshaji wananchi
kiuchumi mpaka kufikia mwaka 2020.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng’i Issa wakati wa ufunguzi wa ripoti ya Tathimini ya Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambao
umefanyika leo jijini Dar es salaam.
“Tunataka
kufikia 2020 watanzania asilimia zaidi ya 70 waweze kushiriki katika shughuli
za kiuchumi ili kufikia katika uchumi wa kati ili kutekeleza sera ya uwezeshaji
wananchi kiuchumi nchini” amesema Issa.
Aidha Issa amesema kuwa watanzania wanatakiwa washiriki katika shughuli za
kiuchumi na wasitegemee zaidi wawekezaji kutoka nje ili kuifanya Tanzania
iendelee kiuchumi kutoka ngazi ya mmojammoja
hadi kufikia maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Kwa
upande wa Meneja wa Utafiti na ufatiliaji wa Sera hiyo kutoka NEEC, Frola
Kajela amesema kuwa Serikali imeandaa sera hiyo ili kuwezesha watanzania
kutumia rasilimiali zilizopo katika kuinua uchumi wa nchi na kuweza kumilikiwa
na watanzania wenyewe.
“Sera
hii inalenga zaidi kwa watanzania kumiliki uchumi wa nchi kwa kutumia
rasilimali zilizopo nchini ili kujishughulisha katika kuleta maendeleo ya nchi
kwa jamii na taifa kwa ujumla mpaka kufikia 2020” alisema Kajela.
Aidha
Bi. Kajela amesema kuwa sera hiyo inafanyiwa maboresho ili kuweza kuwafikia
watanzania wote katika kuelewa na kumiliki uchumi kwa kiasi kikubwa katika
kutekeleza mpango wa serikali uliyowekwa
kuhakikisha watanzania wanajiinua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment