Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi akikabidhi moja ya meza ya kusomea kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Halima Dendego.
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Ufundi Mtwara, Paul Kaji akisoma Risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Halima Dendego.
Wanafunzi wa Shule ya Ufundi ya Mtwara wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Halima Dendego alipokuwa akiongea nao wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya madawati na Benki ya Posta.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Dkt Khatibu Malimi Kazungu akizungumza na wanafunzi wa shule ya Ufundi ya Mtwara.
MkuMkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Halima Dendego akitoa neno la Shukrani kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Halima Dendego akiwa katika picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, baada ya makabidhiano ya vifaa hivyo vya elimu. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Tawi la TPB Mtwara Norbert E. Mbarouk na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Dkt Khatibu Malimi Kazungu. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego amewakata wanafunzi wa shule ya sekondari Mtwara Ufundi iliyopo katika Manispaa ya Mtwara mikindani kuongeza juhudi na maarifa katika masomo yao ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Wito huo umetolewa jana na Mkuu huyo wakati wa zoezi la kukabidhi msaada wa Madawati 45 na Meza 45 yaliyotolewa na Benki ya Posta Tawi la Mtwara (TPB) ikiwa ni juhudi za kuunga mkono Serikali katika Sekta ya Elimu Mkoani hapa.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa wanafunzi hao wanapaswa kujitathimini wao wenyewe kwa kuangalia kitu ambacho kimewaleta shuleni na kufundishwa na Walimu wao jambo ambalo litawasaidia kufanya vizuri katika mitihani yao.
Vile vile Dendego ameishikuru TPB kwa kuguswa na zoezi hilo kutokana na kutambua umuhimu wa Elimu ili wanafunzi hao waweze kujifunza vizuri katika masomo yao.
“Tunaishukuru sana benki ya Posta kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya Elimu katika Mkoa wetu kwa sababu Mkoa huu ulikuwa na upungufu wa Madawati 28937 kwa shule za Sekondari ambapo kwa sasa tuna Madawati 35228 ambayo ni sawa na asilimia 121.7 kwa shule za msingi tuna Madawati ya zaidi ya 500 na sekondari ni 5390,” alisema Dendego.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi alisema kuwa Madawati hayo gharama ya kiasi cha fedha Shilingi Milioni 6 huku akisema kwamba hadi sasa wana jumla ya matawi makubwa 30 na madogo 30 hapa Nchini.
Pia aliongeza kuwa Benki hiyo imekuwa ikitoa fursa mbalimbali za Kiuchumi kwa wananchi kwa kuwawezesha kujiwekea akiba huku wakijikita zaidi na kuhakikisha wanaanzisha huduma za kuwafik
0 comments:
Post a Comment