September 26, 2016

TBL GROUP YANG’ARA WIKI YA USALAMA BARABARANI GEITA



Afisa mawasiliano ya mambo ya nje wa TBL Group, Amanda Walter, akipokea cheti cha uchangiaji wa shughuli za wiki ya Usalama Barabarani kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni,kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya Nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika mkoani Geita.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi kutoka Kitengo cha Usalama barabarani cha Jeshi la Polisi.


***************

KAMPUNI ya TBL Group imetunukiwa cheti kutokana na mchango wake mkubwa katika kuendesha kampeni za Usalama barabarani nchini ikiwemo kudhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani mwaka huu ambayo imezinduliwa  kitaifa mkoani Geita.

Cheti hicho kutoka serikali kilitolewa na Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyojumuisha viongozi na watumishi wa serikali wakiwemo wawakilishi kutoka makampuni na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali.

Akiongea baada ya hafla hiyo,Afisa Mawasiliano ya Nje wa TBL Group,Amanda Walter,alisema kuwa TBL Group imekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeni za Usalama Barabarani na kudhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani na itaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kufanikisha kampeni hizi kwa lengo la kupunguza matukio ya ajali nchini. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
“Mwaka huu mbali na kutoa stika na vifaa vingine vya uhamasishaji tunalo gari maalumu la kupima afya za madereva bure ambalo liko hapa Geita na litaendelea kuzunguka sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.Natoa wito kwa madereva kujitokeza kupima afya zao na kupatiwa matibabu”.Alisema Walter.

Aliongeza kuwa mbali na kupima afya za madereva kampuni imeandaa mafunzo mbalimbali endelevu kwa ajili ya masuala ya usalama kwa  wafanyakazi wake  na makundi mbalimbali kwenye jamii ikiwemo mafunzo ya kuhamasisha unywaji kistaarabu lengo kubwa likiwa ni kuleta mabadiliko kwa watumiaji wanaotumia vinywaji vyenye kilevi  wasiathirike kwa kutumia vinywaji na kuleta athari nyinginezo zitokanazo na ulevi kama vile ajali za barabarani.

Amanda pia alisema kuwa kampuni kutokana na kutekeleza na kuzingatia kanuni za usalama hivi karibuni ilishinda tuzo mbalimbali za usalama moja wapo ikiwa tuzo ya usalama sehemu za kazi inaotolewa na taasisi ya OSHA ambapo pia ilishinda tuzo a kimataifa ya Usalama ijulikanayo kama NOSA.

Wakati huohuo, gari la kupima afya za madereva la zahanati mwendo limekuwa moja ya kivutio kikubwa katika uzinduzi wa kampeni za Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani ambapo madereva wengi na wananchi walijitokeza kwa ajili ya kupima afya zao na kupatiwa matibabu.

Baadhi ya wananchi waliofika kwenye uwanja wa Geita na kushuhudia huduma za upimaji wa afya kwa madereva wameipongeza TBL Group kwa kuanzisha huduma hii ambayo itawawezesha madereve wengi kupima afya zao “Unajua madereva tumekuwa hatuna muda wa kwenda katika vituo vya afya kupima afya ila kwa njia hii ya basi linalotembea tutafikiwa wengi”.Alisema Josephat Ngosha dereva wa malori na mkazi wa Geita mjini.

No comments:

Post a Comment