SHIRIKA la ndege la Precision
Air, limerudisha rasmi safari zake za kuelekea HAHAYA – nchini Comoro kuanzia
leo tarehe 27 Septemba 2016. Ndege kuelekea komoro iliondoka saa 4 asubuhi kuelkea
HAHAYA na ilitarajiwa kuwasili huko saa 5 Asubuhi.
Precision Air ilisitisha
safari hizo mnamo mwaka 2014 na kutangaza kuzirejesha mapema mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumzia kurejeshwa kwa
safari hizo Mkurugenzi wa Biashara wa shirika hilo Bw. Robert Owusu amesema
kuwa Precision Air imejipanga kutoa huduma ya uhakika ya usafiri wa anga kati
ya Tanzania na Comoro, ambayo itarahisisha biashara na safari kati ya nchi
hizo.
“Safari zetu zitakua kila siku
ya Jumanne, Alhamisi na Jumamosi. Na ratiba hii imepangwa makhususi kukidhi
mahitaji ya safari za Kiserekali, Kibiashara na hata zile za mapumziko na kulingana na mapokeo ya soko tunatarajia
kuongeza safari zaidi.” Bw. Owusu amedokeza.
“Tunafuraha kurudisha safari hizi kama tulivyo
ahidi , nah ii itakua sehemu ya 13 katika mtandao wetu kwa ujumla na ni ya pili
kwa safari zetu za kikanda. Nimatazamio yetu kutengeneza mtandao wa safari
ambao utawawezesha abiria wetu kuunganisha safari zao ndani ya Afrika
Mashariki, Africa na Duniani kwa ujumla.
Tunajivunia kuwa na mtandao bora
ziaidi unaowapa wateja urahisi wa kuunganisha safari zao na hatutachoka
kuuboresha kuhakikisha tunaendana na matakwa ya soko.” Bw. Owusu amefafanua
zaidi.
Precision air ndilo shirika
pekee la Kitanzania lilo chini ya umoja wa Mashirika ya Ndege Duniani IATA na
hivyo huwawezesha abiria kufanya booking zao na kuunganisha na mashirika
mengine ya Kimataifa.
Kwa safari za ndani Precision Air inasafiri kwenda sehemu
13 ikitokea Dar es Salaam kuelekea Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Bukoba, Musoma,
Tabora, Kigoma, Mtwara, Zanzibar and Pemba.
No comments:
Post a Comment