Meneja mawasiliano ya ndani wa kampuni ya TBL group,Zena Tenga
(wa kwanza kulia) akisalimia na watendaji wa kituo kulelea watoto
walemavu cha Human Dream Children Village,Emanuel Komba kushoto ni mama mlezi
wa kituo hicho,Celina Fransis na kulia ni Meneja wa mawasiliano ya nje wa
kampuni hiyo Amanda Walter
Meneja mawasiliano ya ndani wa kampuni ya TBL group,Zena Tenga (wa pili
kulia) akimkabidhi moja ya kiroba cha chupa zilizovunjika kwa ajili ya ujenzi
wa uzio Mkurugenzi msaidizi wa Kituo cha kulelea watoto walemavu cha Human
Dream Children Village,Emanuel Komba kushoto ni mama mlezi wa kituo
hicho,Celina Fransis na kulia ni Meneja wa mawasiliano ya nje wa kampuni hiyo
Amanda Walter
Mkurugenzi msaidizi wa kituo cha kulelea watoto walemavu Human Dream
Children Village,Emanuel Komba akiwaonyesha mazingira ya kituo hiko baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni ya TBL group kutembelea kituo hiko na kukabidhi msaada
wa vipande vya chupa vya kutengenezea uzio wa kituo hicho
Mkurugenzi msaidizi wa kituo cha kulelea watoto walemavu Human Dream
Children Village,Emanuel Komba(kulia) akiwaonyesha mmoja wa watoto wanaolelewa
katika kituo hicho baada ya baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TBL group
kutembelea kituo hiko na kukabidhi msaada wa vipande vya chupa vya kutengenezea
uzio wa kituo hicho. BOFYA HAPA KUZOMA ZAIDI.
***************
KITUO cha kuwahudumia watoto wenye ulemavu cha Human Dream
Children Village kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambacho
kimekuwa kikikabiliwa na changamoto ya matukio ya wizi kimepata msaada wa
vipande vya chupa kwa ajili ya kuimarisha uzio wake kutoka kampuni ya TBL
Group.
Msaada huo kwa kituo hicho ni moja ya mkakati wa kampuni ni moja ya
mkakati wa kampuni wa kutekeleza kanuni ya afya na usalama ambayo mbali na
kulenga maeneo ya kazi inalenga pia kwa jamii kwa ujumla.
Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga,alisema kuwa moja ya sera ya
kampuni inatoa kipaumbele kutekeleza suala la Afya na Usalama kuanzia kwa
wafanyakazi ,wageni wanaotembelea viwanda vyake,wateja na jamii kwa
ujumla.
“Kutokana na sera ya
Afya na Usalama tumeguswa na tatizo la kituo hiki la kutokuwa na usalama
ndio maana tumeamua kuwaletea vipande hivi vya chupa vya kuweka kwenye
kwenye uzio kwa ajili ya kuimarisha usalama.Vilevile moja ya mkakati wa
kampuni ni kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto
mbalimbali za kijamii”.Alisema Tenga.
Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa kituo hicho Emmanuel
Komba,ameishukuru kampuni ya TBL msaada huo ambao alidai utasaidia kuondokana
na changamoto ya matukio ya wizi na kuhatarisha usalama wa watoto wanaoishi
kituoni hapo. "Tunashukuru kwa msaada huu mkubwa kwa kuwa utasaidia
kuimarisha hali ya usalama hapa kituoni".Alisema Komba
No comments:
Post a Comment