September 23, 2016

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF) WATOA ELIMU KATIKA MKUTANO MKUU WA 32 WA ALAT MJINI MUSOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Geprge simbachawene akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF Bw. Sebera Fulgence kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wanyakazi (WCF) alipotembelea banda la Mfukohuo, pembezoni mwa mkutano mkuu wa mwaka wa ALAT mjini Musoma

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), umetoa elimu kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu Mfuko kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu 32 na Tuzo za viongozi wa Serikali za Mitaa (Mayors Award), mjini Musoma mkoani Mara.
Mkutano huo ulioanza Septemba 22 na kufunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene Septemba 23, 2016, unatarajiwa kumalizika Septemba 24, 2016.
Akitoa mada kwenye Mkutano huo juu ya shughuli na huduma zitolewazo na WCF, Meneja Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, (pichani juu), alisema, Mfuko umeanza kutoa Fidia kwa Wafanyakazi tangu Julai mwaka huu wa 2016 na kuwahimiza waajiri kupeleka michango yao kama ambavyo Sheria iliyoanzisha Mfuko huo inavyoelekeza.
Wajumbe wamepata uelewa na madhumuni ya uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, majukumu yake, jinsi ya kuchangia na viwango vinavyotakiwa kwa mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/2017.
Pamoja na mambo mengine wamepata fursa ya kupata taarifa kwamba kupitia Tangazo la Serikali Na 212A la tarehe 30 Juni 2016, Mfuko umeanza kupokea madai na kulipa mafao kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo yam waka 2015] ikisomwa pamoja na Kanuni za Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi za Mwaka 2016

 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Bw. Sebera juu ya kazi za Mfuko huo
 Maafisa wa WCF wakiwa kwenye banda la Mfuko huo pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa mwaka wa ALAT. Kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, Athumani Khalfan na Zaria Mmanga, wakisubiwri kutoa elimu kwa wajumbe kuhusukaziza Mfuko
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Bw. Sebera juu ya kazi za Mfuko huo

No comments:

Post a Comment