Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia aliposimama
Nangurukuru, wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa njiani kuelekea
mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.
Sehemu ya Wakazi wa Nangurukuru mkoani Lindi wakishangilia ujio wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia alipowasili
kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi
ya siku nne.
**************
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali
itatuma kikosi maalum cha kukabiliana na uvuvi haramu unaoendelea katika bahari
ili kudhibiti na tatizo hilo ambalo limeathiri sana mazalia ya samaki na
kuchangia kupungua kwa samaki baharini.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 7-Sept-2016
wakati akisalimiana na wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi ambao
walijitokeza kumsalimia wakati akielekea mkoani Mtwara katika ziara yake ya
kikazi ya siku NNE mkoani huo.
Makamu wa
Rais amesema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika vizuri serikali pia
itatuma wataalamu wa mazingira ambao watafanya tathmini ya uharibifu wa
mazingira katika bahari ili kujua uharibifu uliofanyika na kuchukua hatua ya
kukabiliana na hali hiyo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Ameeleza kuwa serikali itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu imekuwa ni chanzo kizuri ya mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za uvuvi na shughuli nyingine zikiwemo za utalii.
Ameeleza kuwa serikali itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu imekuwa ni chanzo kizuri ya mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za uvuvi na shughuli nyingine zikiwemo za utalii.
“Bahari yetu ndio
mapato yetu, bahari yetu ndio maisha yetu
tumeitumia vibaya mapato yamepungua na maisha hayawi mazuri hivyo ni
muhimu tuitunze ili iendelee kutulea kwa manufaa mazuri.”
Kuhusu
uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Kilwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti zinazolenga
kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma bora za afya katika ngazi
zote.
Amesema
mpango huo wa uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini utaenda pamoja
na utoaji wa elimu bora wa wanafunzi kote nchini chini ya mkakati wa serikali
wa kutoa elimu bure kuanzia wanafunzi darasa
la kwanza hadi kidato cha nne.
Katika ziara
yake mkoani Mtwara, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan kesho 8-Sep-16 atazindua
jengo la ofisi za Tume ya Maadili ya
Uongozi wa Umma Kanda ya Kusini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
mkoani humo.
Makamu wa
Rais tayari amewasili mkoani Mtwara na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa
mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego pamoja na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela
Kairuki.
No comments:
Post a Comment