Baadhi
ya madaktari wa Zahanati Mwendo na Maofisa wa TBL Group wakijiandaa kupokea
wageni wanaotembelea zahanati hiyo
Baadhi ya
madereva wakipima afya zao
Viongozi
wa serikali wakipata maelezo jinsi huduma za afya zinavyotolewa katika Zahanati
Mwendo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani mkoani
Geita
Huduma ya
Zahanati Mwendo ambayo imebuniwa na kampuni ya TBL Group katika maadhimisho ya
Wiki ya Nenda Kwa Usalama barabarani kwa ajili ya kupima afya za madereva
imekuwa kivutio kikubwa mkoani Geita ambako maadhimisho haya yamezinduliwa
kitaifa na idadi kubwa ya madereva na wananchi wanaendelea kujitokeza kupima afya
zao kwa wingi na kupatiwa matibabu na ushauri nasaha.
Madaktari
maalumu waliopo kwenye gari la kufanyia vipimo la Zahanati Mwendo muda wote
tangia kuwasili mkoani Geita wamekuwa na kazi kubwa ya kutoa huduma
kwa madereva wengi na wanaendelea kujitokeza kufanyiwa vipimo siku hadi siku.
Meneja
Mawasiliano wa TBL Group ,Amanda Walter,amesema inavutia kuona watanzania
wengi wanahitaji huduma ya kupimwa afya na kumekuwepo na mwitikio mkubwa
wa madereva na wananchi wanaotembelea Zahanati Mwendo.
Alisema pia
kuwa wananchi wengi wamejitokeza katika semina ya Mafunzo ya Unywaji wa
Kistaarabu yaliyofanyika katika kituo Kikuu cha mabasi cha Geita ambapo
walipata fursa ya kujua madhara ya matumizi ya vinywaji vyenye kilevi
kupindukia.
''Wiki ya
Usalama ya mwaka huu imekuwa na mwamko mkubwa hususani wananchi walivyojitokeza
kwa wingi katika mafunzo haya ya Unywaji wa Kistaarabu na mengine yanayohusina
na Usalama barabarani.TBL Group tunaendelea kushirikiana na serikali na wadau
wengine katika kampeni za Usalama kwa lengo la kupunguza matukio ya ajali
nchini”Alisema.
Rehema
Nyoki,mkazi wa Geita ambaye amehudhuria mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu
akiongea kwa niaba ya wenzake aliipongeza kampuni ya TBL Group kwa kuendesha
semina za uhamasishaji unywaji kistaarabu na alitoa ombi mafunzo
hayo yafikishwe sehemu mbalimbali nchini kwa kuwa ipo idadi ya waathirika wengi
wa kutumia vinywaji vyenye kilevi kupita kiasi kwenye jamii ambao
wanaishia kupata matatizo ya kila aina.
No comments:
Post a Comment