Washiriki
wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha baada ya mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana. warembo hao wanataraji kupanda jukwaani
Septemba 9, 2016 katika Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro
Warembo wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwandaaji wa shindano la Miss Ilala 2016, Tickey Kitundu akizungumza na waandishi wa habari.
Mwandaaji
wa shindano la Miss Ilala 2016, Tickey Kitundu (walioketi katikati)
akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana kuhusiana na
maandalizi ya shindano hilo litakalo fanyika Septemba 9 mwaka huu. Walio
keti wengine ni Mtaribu wa Shindano hilo, Suzan Okayo (kushoto) na Mkuu
wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye na nyuma yao ni
Washiriki wa shindano hilo.
**************
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema anataraji
kuwa mgeni rasmi katika shindano la Miss Ilala 2016 linalotaraji kufanyika
Ijumaa Septemba 9 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwandaaji
wa Shindano hilo kutoka Kampuni ya Gogetime Enterprises ya jijini Dar es Salaa,
Tickey Kitundu alisema tayari maandalizi ya shondano hilo yanaenda vizuri.
Kitundu alisema warembo 14 watapanda jukwaani
kuwania taji hilo na tiketi ya kushiriki shindano la Miss Tanzania mwaka huu
pamoja na zawadi mbalimbali nyingine.
“Shindano letu linataraji kufanyika Ijumaa hii
katika Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro na mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema,”alisema Kitundu.
Aidha mbali na mgeni huyo rasmi lakini alisema
shindano hilo litapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii tofauti
wakiongozwa na Rubby.
Kwa upande wa zawadi za washindi, Kitundu alisema
kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha sh milioni moja pamoja na
portable TV kutoka Startimes, huku mshindi wa pili akipata sh 700,000 na
kingamuzi, na mshindi wa tatu akipata sh 300,000 na kingamuzi pia.
Alisema kuwa mshindi wan ne atapata sh 200,000 na
watano atapata sh 150,000 pamoja na kingamuzi huku warembo wengine watapata
kifuta jasho cha sh 50,000.
Alisema kuwa shindano hilo litakuwa la aina yake
kwakua linatumika pia kuadhimisha miaka 20 ya shindano la Miss Ilala ambapo
washiriki wengine wa zamani wanataraji kupamba shindano hilo.
Amewataja warembo wanaoshindana kuwania taji hilo
kuwa ni Osmunda Mbeyela, Mercy Zephania, Melody Tryphone, Dalena David, Nuru
Kondo, Julitha Kabete, Sporah Luhende, Queen Nazil, Lilian Omolo, Mariam
Maabad, Brenda Allan, Sabrina Halifa, Agriphina Nathaniel na Grace Malikita.
0 comments:
Post a Comment