Mkuuwa Mkoa
wa Mwanza John Mongela (katikati) akikata utepe kuzindua tawi la Rock City Mall
la benki ya NMB jijini Mwanza. Wengine pichani ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
wa NMB, Magreth Ikongo (kulia kwa mkuu wa Mkoa) na Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkurugenzi
Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, pamoja na watumishi wengine wa benki hiyo.
***************
Benki ya NMB imeendelea
kutanua mtandao wa matawi yake nchini ili kuwa karibu zaidi na wateja wake.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, NMB ilizindua tawi jipya la NMB Rock City lililopo
ndani ya jengo jipya la kibiashara la Rock City Mall jijini Mwanza. Tawi hili
linafanya jumla ya matawi ya NMB kwa Mwanza mjini kufikia matano na 28 kwa Kanda nzima ya ziwa nani imani ya NMB zinduzi huu unaleta tumaini jipya kwa
wateja wa NMB jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla.Huduma zinazotolewa na
tawi hili jipya ni pamoja na kufungua akaunti, mikopo, huduma ya fedha za
kigeni, huduma za kuweka na kutoa fedha.
Katika kuhakikisha kuwa NMB
inahudumia makundi mbalimbali ya wateja wake kulingana na mahitaji yao ya
kifedha, wiki iliyopita, benki iliendesha mkutano wa Klabu ya Biashara
uliowakutanisha pamoja zaidi ya wateja 300 wanaohudumiwa na matawi ya NMB ya
jijini Mwanza. Baadhi ya faida zilizopatikana katika mkutano huo ni pamoja na
mafunzo ya jinsi ya kukuza biashara, elimu ya mlipa kodi, jinsi ya kutunza
daftari la biashara na njia mbalimbali za kuboresha biashara.
Meneja wa NMB kanda ya
ziwa- Abraham Augustino akiongea katika mkutano wa klabu ya biashara
uliofanyika jijini Mwanza wiki iliyopita. Zaidi ya wateja 300 walihudhuria
mkutano huo ambapo pamija na mambo mengine walipata mafunzo ya jinisi ya kukuza
biashara, elimu ya mlipa kodi na njia mbalimbali za kuboresha biashara.
Mjumbe wa Bodi ya
Wakurungezi ya NMB- Margaret Ikongo akizungumza katika mkutano wa Klabu ya
Biashara jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment