Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wa pili kulia), akishirikiana na viongozi wengine
akiwemo Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (kushoto), na Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omar Kumbilamoto (katikati) kuzindua ujenzi
wa kituo cha polisi kinachojengwa katika Jimbo la Segerea ikiwa ni mkakati wa
kupambana na uhalifu katika jimbo hilo.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akishiriki
ujenzi wa awali wa kituo cha polisi kinachojengwa katika Jimbo la Segerea ikiwa
ni mkakati wa Mbunge wa jimbo hilo kupambana na vitendo ya uhalifu katika jimbo
hilo.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(suti nyeusi),
akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya Ujenzi wa Kituo
cha Polisi .Naibu Waziri huyo pia aliongoza Harambee ya Ujenzi wa kituo hicho
ikiwa ni mkakati wa Mbunge wa Jimbo hilo
Bonnah Kaluwa, kupambana na matukio ya
uhalifu.Naibu Waziri huyo aliongoza
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza
wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi .Wa kwanza kulia ni Mbunge wa
Jimbo la Segerea,Mheshimiwa Bonnah
Kaluwa. Ujenzi wa kituo hicho ni mkakati wa kupambana na matukio ya uhalifu
yanayotokea katika jimbo hilo.
Mbunge
wa Jimbo la Segerea la Segerea, Bonnah Kaluwa, akimuongoza Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(suti nyeusi) na viongozi wengine
kwenda kutembelea eneo ambapo ujenzi wa
kituo cha polisi katika jimbo hilo umeanza ikiwa ni mkakati wa kupambana na
matukio ya uhalifu jimboni hapo.
Wananchi
wa Jimbo la Segerea, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi ikiwa ni mkakati
wa Mbunge wa Jimbo hilo, Bonnah Kaluwa, kupambana na matukio ya uhalifu katika
jimbo hilo. (Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment