August 16, 2016

KUSHEREHEKEA MIAKA 100 YA NYWELE ZA KIAFRIKA

 Warembo wakigawa viwanywaji wakati wa sherehe hiyo.
 
 Read Carpet
 Burudani kutoka kwa Hadija Kopa
ZAIDI ya watu mia mashughuri walifika katika kusherehekea miaka 100 ya nywele za Kiafrika, shughuli hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti Ulikuwa ni uzinduzi wa kipekee. 

Na yote ni kuhusu uwezeshaji wa mwanamke wa Kiafrika. Mandhari ya shughuli hii ilikuwa ni "Kila ndoto ni halali" Usiridhie Darling Group, kama kiongozi wa soko la nywele na biashara za huduma ya nywele Afrika , walitambulisha bidhaa zao mbalimbali za Aliyana professional kwa watengeneza nywele wote nchini Tanzania. 

Tukio hilo pia lilipambwa na wanamitindo mahili wa Tanzania Wakati maonesho ya mavazi yakiendelea, wageni walitambuliswa mfululizo za bidhaa za nywele za Aliyana Professional Shine na Aliyana Professional enrich zenye ubora wa hali ya juu katika kuimarisha nywele. 

Wanamtindo walipewa nafasi ya kuingiliana na watengeneza nywele hodari ambao Tanzania inaweza kujivunia nao. Tukio hilo lilibarikiwa na uwepo wa mwakilishi wa Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nnauye. 

Ambaye ni Mkurungenzi Idara Ya Sanaa na Utamaduni, Leah Kihimbi. Mwakilishi mwandamizi wa kampuni hiyo hapa Tanzania, alizungumza kuhusu kundi hilo changa la Godrej Group lenye miaka 119 likiwa na uongezeko la uwepo wake barani Afrika, Amerika ya Kusini, na Asia. 

Kundi hilo la Godrej Group ni wamiliki wa Darling Group katika nchi 14 za Afrika, ambapo Darling ni kiongozi wa soko la nywele na huduma za nywele. Msemaji wa kampuni hiyo aliwakaribisha wageni waalikwa kuwa sehemu ya safari hii ya kusisimua nchini Tanzania, sababu bidhaa mbalimbali za Aliyana Professional ni kutoka katika uimara huo.

No comments:

Post a Comment