Nafasi Ya Matangazo

August 01, 2016

Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya warembo 13 kutoka mikoa minne ya Kanda ya kaskazini Jana wameingia rasmi kambini kwa ajili ya kujiandaa katika shindano la kumtafuta mlibwende Wa kanda ya kaskazini.

Akizungumza na waandishi Wa Habari muandaaji Wa shindano hilo Mkurugenzi Wa kampuni ya mwandago investment Faustin Mwandago alisema teari maandalizi yote yamekamilika na warembo wote 13 kutoka mikoa ya Arusha ,Manyara, Kilimanjaro na Tanga wameshaingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na shindano hilo.

Alisema kuwa anauwakika kabisa taji la mrembo Wa Tanzania ambalo adi sasa bado linashikiliwa na mrembo kutoka kanda ya kaskazini mkoani Arusha Lilian Kamazima watalitetea na litabaki kwakuwa warembo wake ni wazuri na wanajiamini vyakutosha pamoja na nithamu ya hali ya juu.

Alisema pia katika shindano la mwaka huu wamechagua warembo ambao wanauelewa wa kutosha na wanajitambua hivyo wanaamini kabisa taji litabaki kanda ya kaskazini.

"Mashindano ya mwaka huu ni tofauti na shindano hili nilakipekee kwani tumeboresha mambo mengi sana kuanzia burudani ,warembo wenye na hata ulinzi tumeweka historia ya kutoa miss Tanzania na aitaishia apo tutaendelea kuwatoa warembo kanda hii mpaka watu wachoke maana kanda ya kaskazini inawasichana wazuri wenyesifa zote za kuchukua hili taji "alisema Mwandago.

Aidha alibainisha kuwa warembo watakaa kambini kwa muda Wa siku sita adi Siku ya Augast 6 pale shindano hili litakapo fanyika katika viwanja vya ukumbi Wa triple A Jijini hapa.

Alibainisha kuwa katika shindano hili la kumsaka mrembo Wa kanda ya kaskazini(miss kanda ya kaskazini)bendi ya Fm Academia inatarajiwa kutoa burudani ambapo alisema kuwa bendi hiyo imejipanga kuwapagawisha washabiki wake kwakuwa burudani safi pamoja na staili mpya za bendi hiyo.

Alitaja wathamini waliothamini onyesho hilo hadi sasa kuwa ni clous view hotel ,Geo Security 'Mery saloon ,libeneke la kaskazini blog,Triple A fm pamoja na mwandago investiment .

Aliongeza kwa kuzitaka kampuni mbalimbali kujitokeza kuzathamini shindano hili kwani nafasi bado zipo .
Alitaja viingilio vya onyesho hilo kuwa V.I.P itakuwa shilingi elfu 30000 huku kawaida ikiwa shilingi 10000.
Posted by MROKI On Monday, August 01, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo