Meneja Mkakati na Ubunifu, Samuel Dyamo (kulia) akimkabidhi Katibu
Tawala wa wilaya ya Ubungo, James Mkumbo sehemu ya madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya DCB kwa shule ya Msingi Kimara B. Makabidhiano hayo yaklifanyika jana shuleni hapo.
Meneja Mkakati na Ubunifu, Samuel Dyamo (kulia) na Katibu
Tawala wa wilaya ya Ubungo, James Mkumbo wakifurahia baada ya makabidhiano ya madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya DCB kwa shule ya Msingi Kimara B.
Katibu
Tawala wa wilaya ya Ubungo, James Mkumbo akikabidhi msaada wa madawati kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kimara B, Zuxine Mponda.
Wageni wakipiga picha na wanafunzi
Wanafunzi wakiwa wameketi kwenye madawati hayo.
BENKI ya DCB imekabidhi msaada wa madawati 100 kwa
Shule ya Msingi Kimara B, iliyopo Wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam.
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki hiyo, Meneja Mkakati na Ubunifu, Samuel Dyamo, alisema tayari
benki hiyoimesha omba leseni ya kufungua matawi mikoani lakini itaanza kufungua
tawi hilo mkoani Dodoma ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuhamia mkoani
humo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Aidha akizungumzia msaada huo wa madawati 100 kwa
shule ya Msingi Kimara B, iliyopo Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, ni
katika moja ya jitihada za kuunga mkono juhudi za serikali la kuhakikisha kuwa
inaboresha mazingira ya kusomea kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari
nchini.
Dyamo alikabidhi madawati hayo kwa Katibu Tawala
wa wilaya ya Ubungo, James Mkumbo aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Humphrey
Polepole na kusema kuwa benki hiyo ni yawananchi wa Dar es salaam hivyo msaada
huo ni sehemu ya kurejesha kile walichopata kwa wananchi.
“Benki hii ni ya wananchi wa Dar es Salaam, na
wamiliki wa Beki hii ni kutoka Manispaa zote za jiji hili, hivyo tumeamua
kuunga mkono jitahada za serikali katika kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anaeketi
chini,”alisema Dyamo.
Alisema tangu Benki hiyo ianzishwe miaka 14
iliyopita tayari imesha changia kiasi cha sh milioni 179.2 katika huduma
mbalimbali za jamii ikiwepo elimu.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Katibu
Tawala wa wilaya ya Ubungo, James Mkumbo alisema anaishukuru benki hiyo kwa
mchango wake huo na kuzitaka taasisi nyingine kuunga mkoano jitihada hizo za
serikali.
No comments:
Post a Comment