Nafasi Ya Matangazo

August 25, 2016

Meneja Mkakati na Ubunifu, Samuel Dyamo (kulia) akimkabidhi Katibu Tawala wa wilaya ya Ubungo, James Mkumbo sehemu ya madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya DCB kwa shule ya Msingi Kimara B. Makabidhiano hayo yaklifanyika jana shuleni hapo.
Meneja Mkakati na Ubunifu, Samuel Dyamo (kulia) na Katibu Tawala wa wilaya ya Ubungo, James Mkumbo wakifurahia baada ya makabidhiano ya madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya DCB kwa shule ya Msingi Kimara B.
Katibu Tawala wa wilaya ya Ubungo, James Mkumbo akikabidhi msaada wa madawati kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kimara B, Zuxine Mponda.
Wageni wakipiga picha na wanafunzi
Wanafunzi wakiwa wameketi kwenye madawati hayo.


BENKI ya DCB imekabidhi msaada wa madawati 100 kwa Shule ya Msingi Kimara B, iliyopo Wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Meneja Mkakati na Ubunifu, Samuel Dyamo, alisema tayari benki hiyoimesha omba leseni ya kufungua matawi mikoani lakini itaanza kufungua tawi hilo mkoani Dodoma ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuhamia mkoani humo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Aidha akizungumzia msaada huo wa madawati 100 kwa shule ya Msingi Kimara B, iliyopo Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, ni katika moja ya jitihada za kuunga mkono juhudi za serikali la kuhakikisha kuwa inaboresha mazingira ya kusomea kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini.

Dyamo alikabidhi madawati hayo kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Ubungo, James Mkumbo aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Humphrey Polepole na kusema kuwa benki hiyo ni yawananchi wa Dar es salaam hivyo msaada huo ni sehemu ya kurejesha kile walichopata kwa wananchi.

“Benki hii ni ya wananchi wa Dar es Salaam, na wamiliki wa Beki hii ni kutoka Manispaa zote za jiji hili, hivyo tumeamua kuunga mkono jitahada za serikali katika kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anaeketi chini,”alisema Dyamo.

Alisema tangu Benki hiyo ianzishwe miaka 14 iliyopita tayari imesha changia kiasi cha sh milioni 179.2 katika huduma mbalimbali za jamii ikiwepo elimu.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Katibu Tawala wa wilaya ya Ubungo, James Mkumbo alisema anaishukuru benki hiyo kwa mchango wake huo na kuzitaka taasisi nyingine kuunga mkoano jitihada hizo za serikali.
Posted by MROKI On Thursday, August 25, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo