Afisa Masoko na Utafiti Mkuu
wa AICC Bi.Linda Nyanda akitoa maelezo kuhusiana na huduma zitolewazo na AICC
na JNICC kwa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi SACP Tusekile Mwaisabila akiwa
ameambatana na RSO wa Mkoa wa Lindi.
*******
Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Arusha (AICC) kimeshiriki maonesho ya Nane nane yanayofanyika kitaifa
viwanja vya Ngongo, Mkoa wa Lindi. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe. Sospeter Muhongo yakiwa na kauli mbiu “Kilimo,
mifugo na uvuvi ni nguzo ya maendeleo. Kijana shiriki kikamilifu.
Kupitia maonesha ya Nane Nane
mwaka huu AICC pamoja na tawi lake la Dar es Salaam, Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) inapata fursa ya kukutana na wadau wake na
wananchi kwa ujumla kuwaelezea juu ya huduma zitolewazo na Shirika hilo. Huduma
hizo ni pamoja na utalii wa mikutano, upangishaji wa nyumba za makazi na nafasi
za ofisi kwa upande wa Arusha.
Mkurugenzi wa Manispaa ya
Lindi Bw.Jomaary M. Saturi akisikiliza kwa makini maelezo toka kwa Mkuu wa
Masoko na Utafiti wa AICC Bi.Linda Nyanda, alipotembelea banda la AICC kwenye
maonesho ya Nane nane yanayoendelea Mkoani Lindi
0 comments:
Post a Comment