Wachezji wa Timu ya Taswa Queens wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe lao baada ya hiy kushiriki Bonanza maalumu la Maadhimisho ya Siku ya
Waandishi wa Habari Duniani, lililofanyika kwenye Uwanja wa Luna Park
Jijini Nairobi Kenya Julai 9, 2016, zilitoka sare ya 0-0 katika
muda wa kawaida na kupigiana penati ambapo Taswa Queens wafunga wenzao wa Kenya kwa penati 4-3.
Mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini Kenya, SJAK, Mbais
Criss, akimkabidhi zawadi ya Kombe la mchezaji bora Nahodha wa timu ya
TASWA QUEENS, Lightness Sirikwa Mayeye, baada ya kutangazwa mchezaji
bora aliyejituma katika mchezo wao dhidi ya timu ya SJAK ya Kenya.
Mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini Kenya, SJAK, Mbais
Criss, akimkabidhi Kombe la ushindi Kipa wa timu ya TASWA QUEENS, Somoe
Ng'itu, baada ya timu hiyo kuifunga timu ya SJAK ya Kenya kwa mikwaju ya
penati 4-3 baada ya timu hizo kutoka sare ya 0-0 katika muda wa
kawaida. Timu hizo zilishiriki kwa pamoja katika Bonanza maalumu la
Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, lililofanyika kwenye
Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016.
Kiungo
wa timu ya Taswa Queens, Ester Zelamula (kulia) akimtoka mchezaji wa
Sjak ya Kenya, Mercy Njue, wakati wa mchezo wa kirafiki katika
Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, uliochezwa kwenye
Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016. Katikati ni
Lightness Sirikwa wa Taswa Queens akijiandaa kutoa msaada
Lightness (kulia) akichuana kuwania mpira na Mercy....
Angela Msangi akichuana kuwania mpira na beki wa Sjak Rebecca Magoma.
Katibu
wa Chama cha Waandoshi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) Amir
Mhando akizungumza na wachezaji wa Taswa kabla ya kuanza kwa michezo
hiyo.
Ester Zeamula akifunga penati.
Mlinda mlango wa Taswa Queens akidaka moja ya penati za wapinzani wao.
muda wa kufurahia ulifika
No comments:
Post a Comment